0
MISS Tanzania mwaka 2006 na mwigizaji wa filamu nchini, Wema Sepetu, amesema atamshtaki yeyote atakayetaka kupata jina kubwa kwa jamii kupitia mgongo wa jina lake kama baadhi ya wasanii waliotambulika kwa jamii kupitia jina lake.


Wema alisema baadhi ya wasanii waliopata majina makubwa kutokana na kuwa karibu naye hawana heshima wala fadhila kwake, hivyo hataki kurudia makosa aliyowahi kuyafanya ya kumwamini kila mtu bila kujua malengo yao.


“Kwa sasa najielewa tofauti na zamani hivyo sitaki niwe daraja la kuwatangaza watu na kuwapatia umaarufu kupitia jina langu,” alisema Wema.

Post a Comment

 
Top