0

Hello ndugu yangu msaka hekima ndani ya Madini Media, natamani sana nikusalimu kwa lugha yako ya kikabila…!!, baada ya bidii kuangukia ziro basi turudi zetu kitaifa kupiga stori mbili tatu na kijana adim sana, mkazi wa Arusha na anafanya muziki, jina lake ni Okaluti Candle!

Wataalamu wa muziki wanamtaja Okaluti kama msanii mwenye nidhamu ya kiwango cha juu katika sanaa, kwa jinsi anavoheshimu na kuenenda katika misingi ya kile anachofanya na kujilinda asijikwae katika neno lolote, mwepesi wa kuchunguza maandiko na kujirudi pasipo kusubiri.

Amini kuwa leo ameketi pamoja nami katika meza ya duara ya Madini Media, ili apate kutujuza mengi aliyonayo moyoni kama anavyodai, hivyo sitamfanyia mahojiano zaidi ya kumpa nafasi yeye kufunguka kadri anavoweza, nakualika sasa kuketi pamoja nami ili tuskie toka kwake.

KARIBU OKALUTI,
Ookay asante sana, mi naitwa Okaluti Candle, nafanya muziki chini ya Like My Light! Leo nimetamani kujibu swali la wengi kuhusu mziki wangu, kuwa siendani na game au nashindwa kubadilika kuendana na wakati. Niombe radhi kwa mashabiki wangu, sababu nimekuwa mkaidi kwa ushauri wao na nyongeza ya hapo ni kwamba siwezi badilika kuendana na upepo sijui. Nipo nitadumu kwa misingi na hizi ni nguzo imara juu ya mwamba, sibabaishwi na upepo. Wengine wanadai eti nitabaki maskini, wamesahau kuwa niko tayari hata ikigharimu maisha yangu. Mashabiki na wafuasi wa muziki wangu, sipendi msijue ya kwamba Muziki ni Kirusi au Roho Kamili, usipokuwa makini unakutumikisha.

Mwanadamu anaposhiriki damu ya vampaya ama kwa kungatwa au kuchanjwa, basi hubadilika na kuwa na tabia za vampaya. Katika mabadiliko haya anaweza asijitambue kabisa na anaweza kufanya tukio kubwa la kusikitisha asitambue ni yeye hata anapoambiwa baada ya uvampaya kutulia anaweza kuwa mbishi sana. Hali ya mtu huyu huendelea kuwa mbaya kila siku kwa kadri virusi vilivyomvamia vinavoendelea kukua na kuzaliana ndani ya mwili wake. Kwa sababu tayari ni mwathirika, katika hali ya uvampaya hujikuta anawaambukizia wengine hata ndugu zake na watu wa karibu yake na mwishowe unakuta jamii nzima inayomzunguka wameathirika na kuwa mavampaya.

Kama ilivyo kwa vapaya, vivyo hivyo na muziki ni kirusi au roho kamili inayoweza kumuingia mtu kupitia masikioni au machoni na kumbadilisha hata kumtumikisha. Jiulize unapokuwa Club alafu ikacheza trak ya Juma Nature, hapo kumpata kijana wa kiume ameketi ni nadra sana, au iwekwe Ndi Ndi Ndi ya Jide hakika hakuna wa kike atakaesalia kwenye kiti. Hatari ni pale inapochezwa Muziki ya Darassa mahari popote pale, hakuna cha Pombe wa Magu wala Baba wa Upako, wote hawa wanajirusha pasipo kujali cha cheo, nafasi walizonazo wanazisahau na kuutumikia muziki, na ukiuzima mziki ndipo wanaanza kujishangaa walichokuwa wakifanya.

Hizo ni track za kuparty zinawapelekea watu kupaty pasipo kujizuia wala kujielewa sababu sio wao tena wenye maamuzi bali ni ile roho au kirusi kilichowavamia. Na vipi kuhusu track ya uchochezi, hapo lazima ushuhudie raia wakibeba silaha za kila aina na wakati mwingine wanaandamana kuvamia ofisi husika. Hii ndio sababu kuu ya BASATA kufungia baadhi ya kazi za wasanii zinazoonekana kukiuka maadili husika, maana ukiziruhusu utakuta jamii nzima wanafanya mambo ya ajabu kutokana na kazi moja tu inayokiuka maadili uliyoiruhusu kusambaa. Hii yote ni kwa sababu muziki ni roho kamili inayoweza kumuatack yeyote kwa haraka sana na kuleta madhara makubwa, si kwake tu bali kwa jamii nzima katika wingi wake.

Niseme nini basi juu ya track zinazohusu wanawake na maendeleo na hata sasa tunayaona matunda yake, pongezi kwako malkia wa nguvu. Kushoto kwangu kuna mmoja ananikumbusha ile ya mtoto wa kiume niache nijitume, na wengi waliobahatika kufikiwa na hii track walihamasika kutafuta. Kipindi cha nyuma zimesikika track kama jukumu letu na amka mtanzania ambazo zimewazindua wengi usingizini walipokuwa wakiota kuwa maendeleo yanaletwa na viongozi. Miziki imekuwa ni faraja katika misiba na katika hali ya huzuni, miziki imetumika mara nyingi sana kuimarisha na kuboresha mahusiano ya wanandoa. Kwa habari ya injili, imevuta wengi katika mikutano na makanisani. Miziki imekuwa ni chachu ya furaha katika sherehe na harusi.

Niseme nini basi juu ya hii miziki ya ‘inama kidogo, shika magoti’ kwa kuwa ni kirusi lazima dada zetu watainama tu na kushika magoti, na dakika si nyingi tunaskia wakiwasifia et ‘unanitekenya ukinyonga’. Niwakumbushe tena jamani Muziki ni Roho kamili, unakutumikisha bila udhuru. Sasa na hizi story za chumbani zinatufikiaje huku, au ndo umbea wenyewe, mke na mume wote wanauchonga. Utaskia et eiii, akaja chumbani na kangamoja akaidondosha, basi kitandani sodoma na gomora. Aya huyu nae anambwambia nanii wake chumbani hata nje tunaskia, et ooh ‘gusa nimeshapagawa tena na tena nitawale kiuno’. Hii miziki inaskilizwa na kutazamwa na watoto na vijana wa kiume na wakike, na roho hii inapowaingia huwa inawatumikisha sawa sawa.

Hakuna utumwa mbaya kama kutumikishwa kwa ngono. Utumwa wote hufanyika kwa mwili nje ya mwili, ila ngono ni utumwa unaopenya ndani ya mwili kuidharirisha soft ya uzazi, kisha hupenya katika akili na kumuharibu mtu kisaikolojia. Mabinti hawa utakuta wanabadilika na kuwa na majivuno, huanza kujikweza, dharau nyumbani hata kwa wazazi wao maana hakuna asichokijua km kukatika amejua na tiyari kasifiwa. Kwa wanafunzi, awe wa shule ya msingi, sekondari au chuo, mara nyingi roho hizi zinawafanya washuke kitaaluma na kushindwa kufanya vizuri katika mitihani yao, na hii inawafanya kuendelea kuwa watumwa wa ngono ili wajaziwe vizuri. Kumbuka hii yote chanzo ni miziki.

Hizi roho zitokanazo na miziki ya mapenzi zinapokuingia na kukufanya mtumwa wa zinaa, hapa ndipo pia mshahara wako utakuwa ni mauti na kabla ya kufa ni laana na magonjwa. Hizi takataka kama Kansa na Ukimwi kwani zinaenea kwa njia gani? Vipi kuhusu kubeba na kutoa mimba? Vipi kuhusu madonda ya tumbo sababu ya msongo wa mawazo kisa mpenzi wako sio mwaminifu? Hivi sio wewe ulietusimulia habari za waliouana kisa wivu wa mapenzi? Je kwa hali kama hii kuna usalama gani kwa watoto wetu? Vuta picha, vijana wetu wana hali gani? Maana hawaishiwi kufundishwa tu kupitia muziki, wanahamasishwa na wakifanya kwa bidii wanasifiwa.

I’m so sorry, I can imagine how yo fell! Tuliza sasa mawazo nikupe tiba ya hawa virusi na jinsi ya kuthibiti hizi roho kamili. Tatizo sio muziki hata kidogo, tatizo lipo katika aina ya muziki unaosikilizwa au kutazamwa na mlengwa. Kama ni wasanii basi tuzalishe kazi zenye kuleta matokeo chanya katika jamii, kama walimu tuifundishe jamii kuenenda kimaadili. Tusiweke mbele maslahi, maana laki tano ya show haiwezi kununua roho za vizazi unavyoangamiza kila siku. Kwa upande wa pili, tuache ushabiki wa kipumbavu, kushabikia miziki ya bhangi, madawa, zinaa na matusi. Hata redioni tuombe track za kisiasa, kimaisha, injili na za kuelimisha au kuhamasisha matokeo chanya.

Maandiko yanasena, ‘kinywa cha mtu hutoa yaujazaoyo moyo wake’ na haya ndio yaliyonijenga kwa imani hai, maana isiyo na matendo imekufa. Hii ndio sababu nimeshindwa kuendana na upepo wa game maana mi nimejengwa juu ya mwamba kwa misingi na nguzo imara. Siwezi kuimba maneno ya aibu na kuwavalisha dada zetu vichupi eti kisa nipate air-time na hivyo vilakilaki vya show. Kufanya hivo ni kuua kizazi hadi kizazi maana muziki haufi, bunduki inaua mmoja mmoja ila muziki unaua vizazi HADI vizazi kwa jinsi unavoishi, kukua na kuenea. Ukiweza Download track zangu, zote nimeimba kuhusu maisha na kimaadili zimehaririwa na Like My Light! Zote ziko (HAPA)

OKALUTI CANDLE - ALL TRACKS
Binafsi nimepata kitu kipya, vipi wewe ndugu, maana ni muda mrefu nimekaa pembeni na kumwachia nafasi Okaluti ili kwa pamoja tuthibitishe maneno ya wachambuzi wa sanaa juu ya kile wanachoamini kuwa Okaluti ni mwanamziki mwenye nidhamu sana zaidi ana uwezo mkubwa wa kufikiri.

Nisijue kwako imekuwaje, ila mimi nilikuwa darasani, na sasa nikushukuru wewe ulieketi nami kwenye meza ya Madini Media katika kusikiliza hekima ya Okaluti Candle, zaidi nakusihi usiondoke bila kutembelea vipengele kadhaa katika blog hii, na jitahidikufanya hivo kila siku,


©M(L)30MA17-04
Source:     Okaluti Candle
Editor:      Samson P. Duttu
Allowed:  Share, copy&paste
Don’t try: To edit any.

Post a Comment

 
Top