1
Hello Tanzania...!! Hi kwa ndugu na majirani wa Madini Media. Leo ni siku nyingine tena tunakutana tena ndani ya nyumba ya wanahabari, na kwa leo imenipendeza sana kukidhi haja za wale wanaohitaji KUANZISHA KIPINDI CHA TV.

Ndio, Paschal Mayalla ni mwandishi wa habari wa kujitegemea, anatayarisha vipindi vyake na kuvitangaza kupitia vituo mbalimbali vya Televisheni, Redio na kusambaza habari kwenye Magazeti, zaidi ni mmiliki wa kampuni ya PPR.

Kupitia mtandao wa jf tayari kamimina MADINI kwa wote, hivyo basi nasi hatuna budi kuungana nae katika darasa hili ili tuweze kufunguliwa macho na kuona njia ya kufikia pale tulipotarajia, basi kaa mkao wa kujifunza somo adim sana.

KUANZISHA NA KUENDESHA KIPINDI BINAFSI CHA TV.


1.0 Kwanza uwe na wazo.

Wazo au Program Idea ndio ndio utajiri mkubwa kuliko kitu chochote. Wazo ni kipindi kuhusu nini, maudhui ya kipindi, lento la kipindi ni nini?. Jee ni kipindi cha aina gani na kitaendeshwaje?.

2.0 Aina za Vipindi vya TV.

Kuna aina nyingi za vipindi vya TV.

Kuna TV Documentary, TV Talk Show, TV Reality Show, VOX Pop, TV feature, TV Descriptive, TV Exhibition show, Live TV Prog, TV Interview Prog. etc.

3.0 Mwendeshaji wa Kipindi/Mtangazaji.

Nani atakiendesha kipindi, Mtangazaji, kama ni wewe mwenyewe, jee una kipaji?, una uwezo?, una sauti?, unatazamika (photogenic)

4.0 Mtayarishaji wa Kipindi /Producer


Nani atakitayarisha kipindi?, nani atakitengeneza kipindi?, yaani producers. Wako wa aina Tatu.

4.1 TV Stations

UKipeleka wazo lako kwenye TV yoyote wakiridhia TV hiyo wanaweza kuwa producers na mkakubaliana kugawana mapato, wao watakitengeneza bure na kukirusha bure, kisha hiyo TV wakulipe wewe, au mgawane mapato.

Advantage: The easiest and the cheapest, unachohitaji ni kuwa na wazo tuu hata kama huwezi kutangaza, watakutafutia mtangazaji.

Disadvantage: Wazo linaweza kuibiwa, ama wanaweza kukulalia kwa kulipwa kiduchu!.

Kipindi hicho lazima kirushwe TV hiyo tuu wanayokutengenezea.

4.2 Production House/Studio.
Hizi ni makampuni ya production ambao unapeleka wazo lako, wanakupa gharama za kukutengenezea kipindi chako, unawalipa. Bongo makapuni ya kutengeneza vipindi yako zaidi ya 100.

Advantage: Mkiisha kubaliana bei, kipindi kinakuwa ni mali yako na uko free kukirusha TV yoyote.

Disadvantage: Its an expensive exercise kwa sababu lazima kwanza uwe na fedha za kulipia hiyo production.

4.3 Own Production.

Hii ni baada ya kuwa na wazo, una invest kwenye vifaa, unakuwa na production yako mwenyewe kama mimi nilivyo na PPR.

Hivyo unatengeneza vipindi mwenyewe na kuamua utavirusha wapi.

Advantage: This is the best option, vipindi unateneza mwenyewe na kuvilipia airtime mwenyewe, halafu pesa yote inayopatikana inakuwa ni pesa yako.

Disadvantage: Its an expensive undertaking, lazima uwe na mtaji wa kununua vifaa na viko expensive, na lazima uwalipe watendakazi, ila sio lazima kuanza na kila kitu, unaweza kuanza na baadhi tuu vya muhimu, halafu vingine ukakodisha, kila kifaa kinakodishika na gharama ni cheap kukodi kuliko kutumia pruduction house.

5.0 Vifaa vya Production.

Hivi ni vifaa muhimu kuwa navyo as Basic Equipments za Own Production

5.1 Professional Camera 1 kwa kuanzia ila standard ni kamera 3. Simple ni Milioni 2, expensive ni hadi milioni 100

Kadri unavyotumia kamera nzuri, kipindi kinakuwa kizuri zaidi. Kamera nzuri ni Sony HDV ila hata SLR (hizi za still kama

Canon na Nikon zina video na zinaweza)

5.2 Uwe na Mic nzuri 500,000 - 2,000,000 (wireless)

5.3 Taa angalau 2, 100,000-500,000 (kwa kuanzia sio lazima sana mfano mimi vipindi vyangu vingi, navifanya nje kutumia natural light, mwanga wa jua ambao ni bure.

5.4 Editing bench ni computer ya kueditia hata any good laptop can do. Computer zinazoongoza kwa kupiga kazi ya production ni Mac (apple) ila hata Windows za kawaida zinaweza, kinachohitajika ni high specs tuu kwa upande wa graphic card

Apple ya bei poa ni 1.5 used mkononi

Vifaa vyote vipya na used vinapatikana. Vyote vina faida zake na hasara zake.

Vifaa vipya vina faida moja,
vina uhakika na vina guarantee. Hasara ya vifaa vipya ni kwanza ni ghali, lakini pia vingi ni famba za kutoka China na Dubai hivyo havidumu.

Vifaa used, vina faida mbili, kwanza bei yake ni cheap, pili ni vifaa genuine vya ukweli ila tatizo lake havina guarantee na vingine technology yake imepitwa na wakati.

6.0 Gharama za Airtime.

Ukifanikiwa kuanzisha studio yako na kutengeneza kipindi, ili kirushwe lazima kufanyike mambo matatu yafuatayo

6.1 Kipindi Kinunuliwe na TV Station.
Ukiishatengeneza kipindi chako, unawauzia TV Station, wao wanakupipa kiasi unachotaka na kukirusha kipindi, mapato yote ya kipindi chako ni mali ya TV Station.

Advantage: Kazi yako ni kuzalisha tuum yaani unauza kipaji, unakama fungu lako kwa ulaini.

Disadvantage: TV zetu zinatubania sana, watakulipa pesa mbuzi kisha wao ndio watazimake, ila TV za hapa wako radhi kulipia mamilioni kununua vipindi vya nje kuliko vya ndani.

6.2 Kipindi kirushwe bure na TV Stations Mgawane Mapato Co-production
Ukiisha tengeneza kipindi chako, unakipeleka TV Station kuomba kirushwe bure, kikipata wadhamini, mnagawana 50/50 na TV Stations

Advantage: Wewe unaingia ghara za kutayarisha tuu, halafu unaingiza fedha za udhamini.

Disadvantage: Ukitokea udhamini mnene, unawafaidisha TV Stations bure.

6.3 Ukirushe kwa Gharama zako.

Ukiisha tengeneza kipindi chako, unakilipia fully kukirusha kwenye TV Station

Advantage: Ukilipia kipindi, unaamua kitoke TV ngapi, unawalipa TV airtime yao wanakurushia, fedha zote ulizopata zinakuwa zako.

Disadvantage:You have to be good kupata mdhamini mzuri atakayelipa pesa za production, airtime na faida ukabaki.

Rates za Kurusha kipindi cha 30 min.
-The cheapest ni TBC -TZS 2,000,000
-The highest ni ITV -TZS 5,000,000



-MWISHO-

Much thanks Mr. Mayalla kwa somo adim sana. Heshima sana kwako pia uliungana nasi mwanzo hadi mwisho wa somo hili. Nina imani kipofu kapewa kuona na kila mwenye nia ya kuanzisha kipindi binafsi cha TV tayari kapewa njia.

Baada ya somo hili linafuata JINSI YA KUPOST KITAALAM KATIKA BLOG, ni hapa hapa kupitia mtandao wa MADINI MEDIA kwenye kipengele cha JOURNALISM. Endelea kuwa pamoja nasi hapa katika JUMBA LA WANAHABARI.

Post a Comment

  1. Amazing work
    But I'm a creative Genius kwenye vpind kuja na idea nzur pia kuandika script za movie nlikuwa nataka Sasa utuelekeze namna nzur ya kupat wazoo zuri Zaid juu ya Tv shows but kiwe kinHamasisha jamiii zetuu

    ReplyDelete

 
Top