0
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga, Zainabu Telack amewataka wasichana kuwataja wanaume waliowakatisha masomo ili hatua za haraka zichukuliwe na kukomeshwa kwa vitendo hivyo katika mkoa huo.


Ametoa changamoto hiyo leo kwenye maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Duniani ambayo kitaifa yamefanyika mkoani Shinyanga.


Wakati wa maadhimisho imeelezwa kuwa watoto wa kike kujiingiza katika mapenzi katika umri mdogo kuna madhara makubwa kiafya na ustawi wa maisha yao kwa ujumla.

Telack amelipongeza Shirika la Agape linalopinga mimba na ndoa za utotoni na kuamua kuwaweka kwa pamoja watoto walioathirika na janga hilo.

Amesema mkoa unaongoza kwa mimba na ndoa za utotoni kwa asilimia 59 kutokana na sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mila potofu.

Amewanyooshea kidole wanaume wanaowanyemelea wasichana kwa kuwa wazazi wamekuwa wakiwasomesha kwa shida, lakini wao huibuka na kuwaharibu na kisha kuwatelekeza baada ya kuwaharibia maisha.

amezindua kituo cha kuwapatia elimu watoto wenye kuathirika na mimba na ndoa za utotoni kilichopo kata ya Chibe, Manispaa ya Shinyanga.

Kaimu Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali linalopinga mimba na ndoa za utotoni la Agape, Samwel Magina amesema mpaka sasa wanawaathirika wa mimba na ndoa za utotoni 117 na kuwapatia elimu ya masafa ya kidato cha kwanza, pili na tatu na wengine Chuo cha Maendeleo ya Jamii.

Post a Comment

 
Top