0
Kauli ya Rais Mstaafu, Dk Jakaya Mrisho Kikwete imemfanya aingie kwenye vichwa vya habari wiki hii. Aliitoa wakati akihutubia mbele ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, UDSM.


Akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 55 chuo hicho, katika sehemu ya hotuba yake alisikika akisema, “Ukiwa mpya lazima watu waone una mambo mapya, lakini mapya ya maendeleo, alisema huku akiangalia hadhira inayomtazama huku akitabasamu.


“Sio mapya ya kubomoa ya kule tulikotoka,” aliongeza kwa kicheko na kuendelea na hotuba yake.

Bado haijaweza kufahamika kauli yake ilimaanisha nini. Kikwete ni Mkuu wa chuo kikuu hicho.

Post a Comment

 
Top