0
Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, David Cameron amejiuzulu kama mbunge.



Ametangaza uamuzi huo Jumatatu hii.


Hatua hiyo imekuja ikiwa ni karibu miezi mitatu baada ya Cameron kuachia ngazi kamna waziri mkuu kufuatia kura za Uingereza kujiondoa kwenye umoja wa Ulaya, June mwaka huu.

Akiongea na ITV News, Cameron amedai kuwa alitumia muda kuamua kuchukua uamuzi huo mgumu lakini amedai kuwa angekuwa kikwazo kwa kazi za serikali.

Alikuwa ni mbunge wa Witney na amedai kwamba ilikuwa ni heshima kuliongoza jimbo hilo.

Post a Comment

 
Top