Maafisa wa korea kusini wametahadharisha kwamba huenda Korea Kaskazini ikafanya jaribio jingine la bomu la nyuklia wakati wowote, baada ya kutekeleza jaribio jingine la bomu la nyuklia Ijumaa.
Jaribio hilo la Ijumaa lilikuwa kubwa zaidi kuwahi kufanywa na Korea Kaskazini.
Msemaji wa jeshi la Korea Kusini amesema bado kuna shimo la kulipua bomu ambalo halijatumiwa katika eneo la kufanyia majaribio Punggye-ri ambalo linaweza kutumiwa kulipua bomu la sita wakati wowote.
Korea Kaskazini ilishutumiwa vikali na jamii ya kimataifa baada ya jaribio hilo la Ijumaa na hali ya wasiwasi na uhasama imeongezeka.
- Marekani yatishia kuiadhibu Korea Kaskazini
- Mwanamke maarufu zaidi Korea Kaskazini
Jumapili, mmoja wa maafisa wa jeshi la Korea Kusini alinukuliwa na shirika la habari la taifa hilo Yonhap akisema kwamba nchi hiyo ina mpango wa kuuangamiza kabisa Pyongyang, mji mkuu wa Korea Kaskazini, iwapo kutaonekana dalili kwamba nchi hiyo inajiandaa kutekeleza shambulio la kinyuklia.
Bado kuna shaka kuhusu uwezo wa Korea Kusini kuweka mabomu ya nyuklia kwenye makombora ya masafa marefu, kuiwezesha kutekeleza shambulio, lakini wataalamu wanasema hatua zilizopigwa na taifa hilo zinazua wasiwasi.
Jumatatu, shirika la Yonhap lilimnukuu afisa mmoja wa serikali akisema dalili zinaonesha Korea Kaskazini imekamilisha maandalizi ya kutekeleza shambulio jingine milimani kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Post a Comment