Utafiti umebaini kwamba mkono unaathiri jinsi simu yako inapokea mawimbi.
Utafiti huo unasema simu tofauti hufanya vizuri ikiwa imeshikiliwa kwa kutumia mkono mmoja kuliko mkono mwingine.
Prof Gert Pedersen, kutoka chuo kikuu cha Aalborg anasema kwamba antena (kifaa kinachopokea mawimbi) za simu huwa zimewekwa mahali ambapo binadam hushikilia simu yake, na hivyo kuathiri jinsi simu inapokea mawimbi.
Mkono wa kushoto.
Miongoni mwa simu zinazofanya vyema zikiwa zimishikiliwa kwa mkono wa Kushoto:
- Samsang Galaxy s7 Edge
- Microsoft Lumia 650
- Huawei P9
Mkono wa kulia
Miongoni mwa simu zinazofanya vyema zikiwa zimishikiliwa kwa mkono wa kulia:
- iPhone 6S Plus
- LG G5
- HTC 10
Prof Gert Pedersen anasema ukitumia simu yako bila kuishika kunaimarisha upatikanaji wa mawimbi ikilinganishwa na wakati ambapo umeishikilia.
Post a Comment