0
Idara ya wakimbizi ya umoja wa mataifa UNHCR inasema kwamba wakimbizi wa Somalia nchini Kenya wanaondoka kutokana na vitisho na msukumo kutoka kwa maafisa wa usalama.


Zaidi ya wasomali 300,000 wanaishi katika kambi ya Dadaab, ambayo ni kambi kubwa ya wakimbizi duniani, iliyopo mashariki ya kati ya Kenya.


Maafisa wa Kenya wametishia kufunga kambi hiyo inayotarajiwa kufungwa wakielezea masuala ya usalama wa taifa.

Ofisa wa UNHCR wa Daadab, Mohamed Mahad anasema familia kadhaa zinajiandikisha kurejea makwao wakihofia maisha yao.

Anasema maafisa wa usalama wa eneo hilo wa Kenya wamekuwa wakiawaambia wwakimbizi kwamba lazima waondoke kabla ya kutolewa kwa nguvu wakati kambi hiyo itakapofungwa mwezi huu.

Post a Comment

 
Top