0
Tume ya mazungumzo ya Burundi iliyopewa jukumu la kufuatilia hali ya baadaye ya kisiasa ya Burundi ili kumaliza mgogoro unaoikumba nchi hiyo inasema hivi karibuni inapanga kuwasilisha bungeni matokeo ya kazi yake.


Matokeo hayo yanajumuisha muhula wa rais wa kikatiba, ambao utamuwezesha rais aliye madarakani kugombea muhula mwengine bila marufuku yoyote.


Wanachama 15 wa tume ya mazungumzo ya Burundi inajumuisha wawakilishi watatu kutoka makundi ya kidini, wawili kutoka asasi za kiraia na watatu kutoka vyama vingine vya siasa.

Wachambuzi wanasema kuna uwezekano wa kuondolewa kwa kiwango cha muhula baada ya tume hiyo kuwasilisha rasmi ripoti kwa chombo cha kutunga sheria.

Vyombo vya habari vya nchini Burundi vilisikika vikimnukuu mwenyekiti wa tume hiyo Justin Nzoyisaba akisema kwamba, maoni ya wananchi yaliyokusanywa na tume yake yanaeleza wananchi wanataka kiondolewe kifungu cha katiba kinachoweka kikomo cha muda wa kutawala.

Post a Comment

 
Top