0
Chama hicho cha Kidemocrasia nchini Gabon (PDG) kimekua kikitoa zawadi za simu za mkononi, friji, mashine za kufua nguo na vifaa vinginevyo vya matumizi ya nyumbani katika mji mkuu, Librevelle, kulingana na mwandishi wa BBC idhaa ya kifaransa aliyeko mjini humo.

Rais Ali Bongo (pichani mwenye shati ya rangi ya kijivu) katika kampeni wiki iliyopita

Zawadi hizo zilitolewa katika mkutano wa kisiasa uliohudhuriwa na maelfu ya watu wanaharakati na wafuasi wa chama cha PDG.


Mwanamke mmoja, Naelle, ameiambia BBC:
" Sikuwa na lolote la kufanya, kwa hiyo nilienda. Kulikuwa na msururu mrefu wa watu. Awamu yetu ilipofika, walitupatia zawadi, lakini kwa masharti kwamba tujitambulishe .
Halafu wakatuwekea muhuri kwenye mikono yetu. Nilipokea simu ya Ipad na jirani yangu akapewa friji."

Kwa hiyo kile ambacho watu wanafikiria kwa haya ni moyo wa kutoa.

" Nadhani ilikua hivyo ili tumpigie kura Ali Bongo", mwanamke mwingine kwenye mkutano huo , Gwenaelle, alimueleza mwandishi wetu .

Kiongozi mkuu wa upinzani katika uchaguzi wa Jumamosi ni Jean Ping, mkuu wa zamani wa Kamisheni ya Muungano wa Afrika.

Gabon ni mzalishaji mkuu wa mafuta , lakini theluthi tatu ya raia wake wanaishi katika hali ya umaskini, kwa mujibu wa Benki ya Dunia.

Post a Comment

 
Top