Kampuni ya Bremer Trust ilitangaza jumatano kwamba washabiki wake wanaweza kununua tiketi kwenye mtandao kuanzia Ijumaa kutembelea nyumba yake ya mita za mraba 6,000 ya Paisley Park katika kitongoji cha Chanhassen huko Minneapolis, Minnesota. Uwanja wa nyumba hiyo uliongezwa mara mbili ikiwa ni pamoja na nyumba ya Prince na eneo la ubunifu ambapo alilitengeneza kwa ajili ya kurekodi na utunzi wa nyimbo zake.
Prince Rogers Nelson aliyekuwa na umri wa miaka 57 ambaye staili yake ya muziki wa Rock, funk na R&b akiwa na nyimbo kama "Purple Rain", "Kiss", "1999" na "When Doves Cry" alifariki dunia ghafla nyumbani kwake Paisley Park mwezi wa Aprili. Uchunguzi ulionyesha kwamba madawa ya kupunguza maumivu aliyokunywa kwa bahati mbaya na kuzidi mwilini ya fentanyl yalisababisha kifo chake.
Post a Comment