0
Staa wa Nigeria, Oludemilade Martin Alejo aka YCEE anayetamba na ngoma zake ya Omo Alhaji na Jagabana amepanga kutua Tanzania kwa ajili ya ziara yake ya kimuziki.

YCEE ambaye itakuwa mara ya kwanza kuja Tanzania atafanya mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumatatu tarehe 29th Agosti 2016, ikifuatiwa na ziara ya kutembelea vituo mbalimbali vya habari kuanzia tarehe 29th Agosti 2016 mpaka tarehe 1 Septemba 2016.


Ziara yake ina lengo  la kuungana na mashabiki, wazalishaji wa muziki na wasanii mbalimbali hapa nchini  ili waweze kujenga mahusiano imara zaidi.

“Nina hamu sana ya kukutana na mashabiki wangu wa Tanzania, kwa sababu upendo wanaonipa kupitia mitandao ya kijamii ni wa ajabu na nina furaha sana ya kukutana na watu wapya ” , YCEE alisema.

Msanii huyo wa Omo Alhaji ‘YCEE’ pia ni miongoni mwa wasanii wanaopenda kusaidia jamii kwa kuwafikia vijana wa kiafrika katika masuala ya maendeleo na michezo.

Hivyo katika ziara yake hapa nchini YCEE atatoa msaada wa fedha kwa kituo cha masuala ya umaskini na ukosefu wa upatikanaji wa elimu kwa watoto wa mitaani Kigamboni.

Kigamboni Community Center (KCC) , ni kituo kinacho shughulika na masuala ya kutokomeza umaskini, huku kikijikita katika kutoa elimu ya chekechea na msingi kwa watoto ambao wako mbali na upatikanaji wa elimu.

 KCC pia hutoa fursa nyingine za kujifunza kwa vijana wa Kigamboni, na pia hutoa elimu ya jamii, madarasa ya kuendeleza vipaji na mafunzo ya ufundi stadi. YCEE ameamua kuunga mkono kituo hiki kwa kwa sababu ya kujitolea kwao kukuza vipaji na kujenga upatikanaji wa elimu kwa jamii.

Baada ya ziara yake nchini Tanzania , YCEE ataenda nchini South Africa kuendelea na ziara yake yakukuza na kutangaza muziki wake, na anatarajia kuachia orodha ya nyimbo mpya baadaye mwaka huu utakao fahamika kwa jina la ‘The First Wave‘

Post a Comment

 
Top