Akizungumzia kukamatwa kwa viongozi hao Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu alisema waliokamatwa na polisi kwa ajili ya mahojiano ni Edward Lowassa, Freeman Mbowe, John Mnyika, Dk Vincent Mashinji na Said Issah
“Tulikuwa kwenye kikao cha Kamati Kuu kilichojumuisha wajumbe na wabunge kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya chama. Jumla ya wajumbe walikuwa 170. Tukiwa kwenye kiako walikuja watu wanasema tunatakiwa polisi kwa sababu tumekiuka agizo la lilitokataza mikutano.”
Post a Comment