FID-Q |
Akizungumza na Enewz Fid Q alisema kuwa Rado ni rafiki aliyemfunza kitu katika maisha pasipo kufafanua amemaanisha nini katika sentensi yake hiyo ikiwa hivi karibuni tu ametoa ngoma ”Sihitaji Marafiki” yenye mistari inayoonesha kuwa hana imani na tabia za washikaji.
Rado |
Rado na Fid Q waliingia kwenye mgogoro kuhusu mashairi ya wimbo wa Mwanza mwanza wa fid q ambao Rado alidai aliibiwa mashairi na baadaye akatoa wimbo ulioitwa ‘Usiulize’ ukiwa na mashairi yaliyomdiss FID Q,hata hivyo wakati hili linatokea Fid q alikanusha kuiba mashahiri ya Rado.
Hata hivyo kulikuwa na story kuwa chanzo hasa cha ugomvi huo kilianzia kwenye wimbo wa Fid Q ‘Chagua moja’ ambao unadaiwa mwanzo ulifanyika studio za Baucha records ukiwa na verse ya Rado ,fid Q,Adili na TID kwenye chorus lakini baadaye fid Q alihamisha wimbo huo kwenda kwenye studio ya Bongo records na kufuta mashairi ya rado.
Post a Comment