0
Moja yachangamoto ambayo inawakabili watu wengi ni kwamba ni wazuri sana wa kusema kuliko kuchua hatua, hapa nina maana ya kwamba kila mmoja anapenda kuona matarajio yake yanatimia.

Hata hivyo, kutokana na imani hiyo imepekelekea watu wengi sana kubaki na maisha yale yale kila siku. Unajua ni kwanini? Basi nakusihi ufuatane nami kwani nataka nikijuze siri ambayo watu wengi hawaijui juu ya upangaji wa malengo.

Ipo hivi niliwahi kufanya uchunguzi mdogo katika kazi yangu ya uhamasishaji mahali fulani, moja ya mada ambayo nilikuwa naizungumzia siku hiyo ilikuwa inahusiana na jinsi gani unavyoweza kutimiza  malengo yako na kila mmoja ilionekana kufurahia somo hilo. Kila mmoja wetu ambaye ulikuwepo siku hiyo ilionekana dhahiri anayo ndoto ambayo inasukuma kufikia kilele cha mafanikio.


Ndipo nikachukua jukumu la kutaka kujua kila mmoja aliyekuwepo siku hiyo ni nini ambacho anadhamiria katika maisha yake? Kila mmoja alieleza kwa mapana kutoka na dhamira inavyomsukuma kutoka nafsini kwake. Baada ya kumaliza zoezi hilo la kujua kila mtu lengo lake, ndipo nikawataka watu hao hao waandike kuhusiana na njia ya kutimiza ndoto hizo.


Moja ya maajabu ambayo niliyaaona ni kwamaba watu wengi ni wazuri sana wa kusema nataka kuwa mtu fulani lakini linapokuja suala la utekelezaji wa jambo hilo hapo ndipo ukakasi hujitokeza unajua ni kwanini? Niligungundua ya kwamba watu wengi wana ndoto lakini hawajui mbinu za kutekekeza, hata wale ambao wanajua ni wepesi sana wa kukuta tama.

Ndipo nikawambia ya kwamba kwa jambo lolote ambalo unalitamani liwe kweli ni lazima ujue mbinu ya utekelezaji wa jambo hilo hususani kwa kujifunza na ikiwezekana kulipa gharama, lipa gharama kwa kuwa hakuna maisha ya kimafanikio ambayo hayana gharama.

Pia ikumbukwe ya kwamba katika kujifunza hukohuko kuna changamoto zake, changamoto hizo hizo ndizo ambazo huwafanya watu wachache waweze kuhimili mikiki ya  jambo hilo, na hawa ni watu ambao wamefanikiwa katika sayari hii. Hata hivyo kwa asilimia kubwa ambapo wengi wetu ambao ndio tupo humo huwa hatupo tayari kuvumilia mikikimikiki ya changamato ambazo mara nyingi hujitokeza katika mambo amabayo tunayafanya.

Wengi wetu tupo tayari kuahairisha mambo  na kuleta visingizio visivyokuwa na maana yeyote ile, kwa mfano unakutana na mtu anakwambia anataka kufanya biashara fulani lakini changamoto yake kubwa ni  mataji. Kimsingi ukichunguza changamoto hiyo utagundua ya kwamba ni sababu yatima, nikiwa na maana ya kwamba huna haja ya kuacha kufanya jambo fulani eti kwa sababu ambazo hazina msingi wowote.

Tuende mbele turudi nyuma na kuyatafakari maisha ambayo tunayaishi leo hii, ni kwanini yapo vile vile? Ni wakati wako muafaka ewe msomaji ambaye unasoma makala haya kuweza kutafakari kwa umakini jambo hili japo kwa dakika chache na kuendelea kutafakari juu ya maisha yako.

Tafakari ni kwanini mpaka leo hii hujatimiza malengo yako? Kama umepata jibu, zama tena katika halmashauri yako ya kichwa tafakari tena je unahisi sababu ambazo umezipata ni za msingi au  sio za msingi? Kama umekwisha pata majibu inua macho yako mbiguni, tazama mbigu inavyong`ara kisha tafakari tena na uje na majibu ya kina je unachukua hatua gani kwa hayo yote uliyowaza? Usinibe majibu.

Mmmh, sawa labda nisiendelee kuongea sana, maana naweza nikakupoteza kabisa ila cha msingi ni kwamba tafakari hayo machache kisha uchukue hatua mathubuti za kiutendaji. Hata hivyo nikazie kwa kusema ya kwamba mara zote ukiwa na malengo usiishie kusema tu, bali onyesha njia sahihi za utekezaji. Kufanya hivi kutukupa mwelekeo tosha kwa upande wako kwa kuonesha ni nini! Ambacho unatakiwa kuwa nacho? Na baada ya muda gani!

Huenda bado ukawa haujanielewa nazungumzia masuala ya uwezo wa utekelezaji wa jambo hilo. Maana tunafahamu ya kwamba ili yaitwe mafanikio kuna njia ya kufikia mafanikio hayo kwa mfano kujifunza kutoka kwenye vitabu, video, semina na watu wengine ambao kiujumla wamekwisha fanikiwa. Nikakumbushe kwa mala nyingine kuwa ni lazima uwe na picha kamili ya kule ambapo unataka kuelekea.

Nikushuru sana kwa kusoma makala haya, lakini shukrani zangu zangu zitakuwa zimekamilika endapo utachukua hatua kwa hayo ambayo umekwisha yasoma kwenye makala haya. Nikusihi ya kwamba ulichojifunza mshirikishe mwenzako kama ambavyo mimi nmefanya kwako.

Post a Comment

 
Top