0
Wataalamu wa masuala ya sayansi wanaotafuta maisha nje ya sayari hii, katika anga za juu watahitajika kusubiri zaidi, kwani kuna dalili ya uwepo wa viumbe katika anga za juu wajulikanao kama Aliens.

Mradi wa kutafuta viumbe hao una gharama za zaidi ya dola milioni 100, lakini bado mpaka sasa bado haujapata chochote tangu uzinduliwe,mwaka mmoja uliopita. Shughuli ya kutafuta viumbe hao wa ajabu zinafanywa kwa kutumia darubini kubwa zaidi ambayo inasikiliza dalili yoyote ya kuwepo kwa viumbe aina ya ‘Aliens’ na wengineo.

Darubini hiyo iliyopo West Virginia, Marekani, ni moja ya darubini zenye nguvu zaidi duniani, zenye uwezo wa kutafuta dalili za kuwepo kwa teknolojia ambayo iliundwa na viumbe vilivyo nje ya sayari ya dunia.

Mwaka uliopita mradi huo ulifuatilia nyota lilioenda kwa jina Tabby, ambayo ilikuwa na tabia iliyosababisha watu kufikiri kuwa ilikuwa na viumbe vyenye maisha ndani yake.

Mtazamo wa Idriss Gianni

Mradi wa kwamba Amerika na nchi zingine za Europe zinatafuta Aliens ni uongo. Wao hutafuta mawe ama ukipenda comets na asteroids zenye madini kama dhahabu, mawe ghali ama gesi kama helium ukiongelea comets..

Pia huwa wanatafuta uwezekano wa kuwepo kwa sayari ambapo binadamu anaweza kuishi ili mradi kukaaja kuwa na vita za kinuclear ama mazingira hatari humu duniani wale matajiri watatorokea kule warudi mambo yakipoa..

Kuna uwezekano wa Aliens mle lakini jee wanatufanana ama dimension ukipenda ule mufumo wa maisha yao ni tofauti na vile tunatarajia


Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top