Nafurahi tumekutana tena huku furaha yangu inazidi pale unapotamani kuskia toka kwangu kuhusu uhusiano wa Jicho La Tatu na Paji La Uso.
Huwezi amini kuwa hapa ndipo asili ya neno kipaji ilipatikana na usibishe nitakapokwambia kuwa hapa ndio penye njia ya kuingilia mlango wa sita baada ya ile mitano. Hili ni jicho la ndani, jicho lisioonekana kiimani tunasema ni lango kuu la kiroho.
Kwa dakika chache niruhusu sasa nikupe mafununuo kadhaa, na natamani sana tuangaze kwa mitazamo yote ya kidini au kiimani, kisayansi na kihisia.
HIZI NI SEHEMU ZINAZOONESHA UHUSIANO WA JICHO LA TATU NA PAJI LA USO
1. Third Eye - Thalamus - Eye of Horus
Hapa ni kwa mtazamo wa kisayansi nafikiri ni kwenye somo la anatomy kuhusu ubongo, jicho la tatu linaonekana katikati ya ubongo (zingatia katikati) vertebrate brain hapo ndio zinapozalishwa homoni za kulaza au kuamsha hisia maono usingizi nk.
2. Mathematics
Katika ulimwengu wa mahesabu na hesabu, wanamahesabu kwenye ishu za ratio cos na tan watatusaidia hapa.
4. Baptism & Sijda
Kiimani katika ukristo, kwenye ubatizo alama ya msalaba kwenye paji la uso ndio hukamilisha tendo na kuwa Mkristo kamili sasa.. Lakini pia ukisoma kitabu cha ufunuo na habari za kutiwa Muhuri katika paji la uso utafahamu zaidi..
Kwenye Uislam tunajua nini maana na umuhimu wa swala tano na kuthibitisha uchaji wako katika swala tano ni sigida kwenye paji la uso.
5. A kiss on the Forehead
Kwenye mahusiano busu kwenye paji la uso ni tofauti kabisa na mabusu ya sehemu nyingine yoyote.
6. FREEMASONRY
Kwenye imani za mpinga Kristo freemason satanism nk alama yao kubwa ni jicho la tatu
7. SEVERE PUNISHMENTS (WATERBOARD)
Kwenye adhabu na mateso mbalimbali paji la uso hutumika kuleta adha ya ajabu mwilini... Mateso ya water board ni mfano mmojawapo. Unalazwa chini unafunikwa kitambaa usoni kisha unamwagiwa maji.. Ni aina ya adhabu isiyoumiza mwili bali inayoumiza hisia.
8. Michezoni:
Kwenye mchezo wa ngumi alama za juu ni zile ambazo zinaangukia kwenye paji la uso.
Nimejaribu kwenda na picha kuokoa ufafanuzi wa maneno mengi... Tunaishi kwenye ulimwengu wa ajabu mno.. Tunashiriki kitu hicho hicho lakini kwa maana matumizi na mitizamo tofauti. Tunafundishwa kutolala chali kuepuka ndoto za mauzauza na majinamizi kumbe siri ni jicho la tatu jicho la maono.
Manabii na watenda miujiza hupenda kuwapuliza ama kuwashika watu penye paji la uso na kifuatacho hapo ni mzinga kama si kupiga kelele... Baadhi ya tiba mbadala hutumia paji la uso kama lango la uponyaji.
Wahindi na wahindu kwenye imani zao hujipaka rangi katikati ya macho kama sehemu ya ibada nk.
Jaribu kutafakari kwa hatua hiki kinachoitwa jicho la tatu, paji la uso, imani yako na maisha yako ya kila siku... Mwishowe tunaweza kujikuta tunaabudu paji la uso kwa muktadha tusiojua.
Source, Maarifa ya Mwendokasi
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.