0
MATUMIZI ya dawa za jamii ya vijiua sumu, maarufu kama antibiotiki, imebainika kuwa kwa muda mrefu huweza kusababisha uvimbe kwenye utumbo ambao huweza kusababisha saratani.

Lakini wataalamu nchini hapa wanasema utafiti zaidi lazima ufanyike ili kupata ushahidi zaidi, na hivyo watu wasiache kutumia dawa hizo.


Asilimia 15-20 ya wakazi wa Uingereza wameathirika na uvimbe tumboni.

Mara nyingi watu hawagundui uwapo wa uvimbe huo na hivyo kuchelewa matibabu.

Uvimbe wa aina hii unaweza kusababisha kansa ikiwa matibabu hayatatolewa mapema.

Katika utafiti huu, watafiti walitumia takwimu kutoka kwa wagonjwa 16,600.

Iligundulika kuwa wagonjwa wenye umri wa miaka 20 hadi 39 waliokuwa wakitumia dawa hizo kwa miezi miwili au zaidi, walikuwa na uwezekano mkubwa wa kupata uvimbe wa tumbo.

Ilibainika kwamba uvimbe huo ujulikanao kama adenomas, ulikuja baadaye maishani tofauti na wenzao wa umri huo, ambao hawakutumia dawa hizo za kutibu magonjwa.

Pia wanawake ambao walikuwa wamemeza dawa hizi kwa miezi miwili au zaidi wenye umri wa miaka 40 hadi 59, walikuwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kupata adenoma siku za usoni.

Watafiti hao wanakiri utafiti wao hauwezi kuthibitisha iwapo dawa za kuzuia magonjwa husababisha saratani na wanakiri kuwa bakteria ambao dawa hizi huweza kuua, pia waweza kuchangia kukua kwa uvimbe wa saratani.

Post a Comment

 
Top