0
 Helloo…!! Ndugu na majirani  wa Madini Media.
Unajua, Kukua kwa sayansi na tekinolojia kumesaidia sana kukua kwa sekta mbalimbali duniani kama uchumi, na biashara kwa ujumla. Kukua kwa sayansi na tekinolojia kumechangiwa na ubunifu na uvumbuzi unaofanywa kila siku na wanasayansi duniani.

Biashara ya sasa inakua kwa kasi kutokana na mchango mkubwa wa tekinologia duniani. Miaka ya nyuma watu walikuwa wanatangaza biashara zao kupitia vyombo mbalimbali vya habari kama Tv, na Redio. Mambo ya miaka ya hivi karibuni watu wanatumia zaidi mbinu zingine za kutangaza biashara zao kama kwa kutumia Blogs, Websites, Facebook, Instagram n.k.

SASA, KARIBU NIKUJUZE FAIDA ZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO KUPITIA BLOGS

UNAKUWA NA UWEZO WA KUJUA TANGAZO LAKO LIMEWAFIKIA WATU WANGAPI.
Hii ni faida ya kwanza ya kutangaza biashara yako kupitia Blogs na Websites. Unapotangaza biashara yeyote ile kupitia website au blog unakuwa na uwezo wa kujua idadi ya watu ambao wametembelea au wameshawishika na tangazo lako uliloliweka. Tofauti na redio au tv ni ngumu kujua tangazo lako limewafikia watu wangapi kwa kila linapotangazwa. Kupitia blog au website idadi ya watu walioliona tangazo lako hujioneshabila kificho.

UNATUMIA GHARAMA NDOGO SANA.
Kila mtu anafanya biashara kwa ajili ya kupata faida ya kumuwezesha kuendesha maisha yake na kukuza biashara yake kila siku. Kutangaza bishara kwa kupitia blogsna websites inatumia gharama ndogo sana ukilinganisha na gharama za kutangaza biashara kwa kutumia Redio au TV. Mfano, kwenye TV au Redio,tangazo hulipiwa kwa sekunde ila kupitia blog au website tangazo hulipiwa kwa mwezi au wiki kutokana na makubaliano na muendesha blog. Pia kama utakuwa umefungua blog au website yako mwenyewe utaweza kutangaza bureeeeee bila gharama yeyote ile.

NI RAHISI KUWASILIANA NA WATEJA WAKO MOJA KWA MOJA.
Hii nayo nifaida ya kutangaza biashara yako kwa njia ya blog au website. Unapotumia blog kutangaza biashara yako, wateja wanajuwa na uwezo wa kuwasiriana na wewe moja kwa moja kwa kutoa comments kwenye kila post yako utakayo iposti. Wateja wanakuwa huru sana  kuijua bidhaa yako muda wowote na sehemu yoyote.

INARAHISISHA NA KUOKOA MUDA.

Kutangaza kwa kutumia blog inarahisisha sana mambo, embu tafakari kuhusu mteja anaefanya kazi, je ana muda wa kutazama TV au kusikiliza Redio?. Ukitumia Tv au Redio kutangaza basi ujiandae kuwatangazia watu wasio na kazi ya kufanya ambao wao hukaa nyumbani tu. Matangazo ya kwenye Redio na TV yanaleta tija kwenye vipindi vya usiku tu. Ila ukitumia Blog Au Website mteja anaweza kupata taarifa juu ya bidhaa yako kupitia simu yake au Laptop yake hivyo inaleta maana ya kurahisisha mawasiliano na kuokoa muda wa kukufata moja kwa moja pale unapotoa huduma yako.

Nafurahi kuona umeskia toka kwangu hii siri na kuelewa kuwa nina pendo la dhati kwako na biashara yako. Nikukumbushe kuwa wewe ni moja ya wengi waliotembelea blog hii, vuta picha - lingekuwepo tangazo la biashara yako, ungepigiwa simu na wangapi? Si wangekuwa wengi ee...!! Basi changamkia hii fursa. Ewe msanii, mfanyabiashara na yeyote anaetamani kutangaza au kutushirikisha katika biashara zake au kazi zake au neno lolote, wasiliana na Madini Media utwambie pasipo kuwazia gharama.
Mawasiliano
Mobile: 0768-500450/ 0629-531833
E-Mail: dakikazamadini@gmail.com

Post a Comment

 
Top