0
Wiki hii katika mitandao ya kijamii kuna picha ambazo zimesambaa zikiuonesha mwili wa msichana anaesadikika kuwa amekufa baada ya kubakwa na watu ambao hawajajulikana na kutupwa nje ya eneo la Chuo Kikuu cha Tumaini (Makumira Arusha).


Mwili wa msichana huyo ambaye jina lake halisi linadaiwa kuwa ni Juliana Isawafo, ulikutwa katika bonde la mpunga jirani na chuo hicho majira ya saa 5 asubuhi siku ya Jumatano.


Mmoja wa Viongozi wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo hicho, (jina lake halikufahamika mara moja) ameuthibitishia mtandao wa Radio5 Arusha kutokea kwa tukio hilo.

Bongo5 ilimtafuta Mkurugenzi wa kampuni ya Black Fox, kampuni ambayo ilikuwa inafanya kazi na model huyo hapa jijini Dar es salaam.
black-fox
“Juliana sisi tunamjua kama model wa Black Fox na mimi ni managing director,” alisema Mkurugenzi huyo. “Alikuwa ni model lakini pia alikuwa ni dansa Arusha, sisi kuna mtu alitupigia simu akatuambia kuna mtu wenu amefariki, tukawapigia simu ndugu zake kuthibisha tukaambiwa ni kweli. Kwahiyo sisi kama sisi tufanya mkutano ili tupeleke rambirambi kwa ndugu,”

Pia mkurungenzi huyo alisema issue za model huyo kubakwa azitakuja kufafanuliwa na jeshi la polisi likikamilisha upelelezi wake.

“Kwa sasa hivi jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi lakini tunachojua mwili wake umeokotwa jana asubuhi na watu wanadai amekutwa katika hali ambayo anaweza akawa amebakwa. Lakini mimi nadhani vitu kama vivyo tuliachie jeshi la polisi litakuwa na taarifa rasmi kwa sababu wao watajua nini kilitokea.

Pia mkurugenzi huyo alisema watatoa taarifa zaidi ya nini kinaendelea pamoja na kutangaza nini wameandaa kwa ajili ya kuwapa pole wafiwa.

Katika hatua nyingine mkurugenzi huyo amesema Juliana hakuwahi kufanya kazi na Diamond kama baadhi ya watu wanavyozungumza katika mitandao.

Katika mitandao ya kijamii Alhamisi hii kulizuka uvumi usio wa kweli kuwa model huyo aliyefariki ni yule aliyeonekana katika video ya wimbo Salome wa Diamond Platnumz.

Kwa upande Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema tukio hilo lilitokea jana saa 11:30 asubuhi eneo la Makumira.

Alisema taarifa za awali zinaeleza kuwa Novemba 1 mwaka huu muda wa saa 18:30 jioni marehemu aliondoka nyumbani kwake kwenda kwenye sherehe ya kuzaliwa “Birthday Party” ya rafiki yake ambayo ilipangwa kufanyika kwenye baa iitwayo V. I. C iliyopo eneo la Kilala lakini hakuonekana katika sherehe hiyo.

Siku ya pili Novemba 2, polisi walipata taarifa juu ya kuwepo kwa mwili ambao umekutwa kando ya barabara ya kuelekea Ndolo Lodge, baada ya askari kufika eneo hilo walikuta mwili huo ukiwa mtupu na pembeni yake kulikuwa na nguo zake.

Alisema uchunguzi wa awali ulionyesha kuwa mwili huo ulikutwa na alama za kucha shingoni na uvimbe sehemu za siri kitendo kinachoashiria alikuwa amebakwa.

Alisema hadi sasa chanzo cha kifo hicho bado hakijajulikana na hakuna mtuhumiwa yeyote aliyekamatwa huku msako ukiwa unaendelea ili kuwabaini wahusika wa tukio hilo huku mwili wake ukiwa umehifadhiwa hospitali ya Mount Meru kwaajili ya kufanyiwa uchunguzi wa daktari.

Post a Comment

 
Top