Akiongea Alhamisi hii katika kipindi cha Enewz cha EATV, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Nchini, Joyce Fisoo amesema wamekuwa wakipokea malalamiko tofauti tofauti lakini sio la wasambazaji kuiba kazi za wasanii.
“Kama kuna wambazaji wanaosambaza kitapeli mimi nadhani waondoke kabla mkono wa sheria haujawafuata,” alisema Joyce. “Kwa bahati mbaya ofisi yetu haijapokea malalamiko ya namna hiyo. Tumewahi kupokea malalamiko ya watu ambao hawalipwi fedha zao kwa wakati na wasambaji lakini tumelishughulikia kesi kama tatu, mbili za Mwanza na moja ni ya hapa Dar es salaam. Lakini kama kuna hutuma za namna hiyo, nadhani huu ndio muda wa kutuletea hizo taarifa kwa sababu kila msambazaji anatakiwa kutambua kazi aliyopewa ni jasho la mtu na hapaswi kudhulimiwa kwa sababu ametumia muda wake na pesa,”
Katika hatua nyingine Joyce alisema tasnia ya filamu inashuka kutokana na wasanii wa filamu tofanya utafiti wakutosha wakati wanandaa kazi zao hali ambayo inawapelekea kuandaa kazi ambazo hazina msisimko kwa mashabiki.
Post a Comment