Akizungumza na waandishi wa habari Naibu Waziri Elimu,Sayansi na Teknolojia, Mhandisi Stella Manyanya alisema, “Tumeangalia sifa zifuatazo: fani ya kwanza tumesema awe kwenye fani ya sayansi za tiba na afya, ya pili ualimu wa sayansi na hisabati, ya tatu uhandisi wa viwanda,kilimo, mifugo, mafuta na gesi asilia, sayansi asilia na sayansi ya ardhi,ufanisi majengo na miundo mbinu.”
“Lakini pia tumesisitiza wale wenye mahitaji maalum,kama vile ulemavu na uyatima,lakini hata tukisema kwamba uyatima hatumaanishi yatima mwenye uwezo, maana yake anaweza kuwa amefiwa na mzazi mmoja mwingine yupo lakini pia mzazi aliyetangulia ameacha fursa za kutosha kiasi kwamba hali ni nzuri,huyo tunasema yule ambaye ni yatima maskini,”alisisitiza.
“Vile vile ufaulu, na ufaulu huo uwe katika maeneo yale ya vipaumbele kwa mfano unaweza ukawa umefaulu masomo ya kukuwezesha kuingia kwenye sayansi pengine ufaulu wako hauko wa juu sana, pengine tuchukulie tutaanza na wa division 1, wakishajaa unaingia 2, wakishajaa unaendelea. Kwahiyo hatutaweza kumchukua wa chini wakati mwingine wa juu bado hajapata kwasababu hiyo inatusaidia katika upimaji wa haki,”aliongeza.
Aidha mhandisi Manyanya amesema kuanzia mwaka huu wa masomo wanufaika wote wa mikopo watakopeshwa kulingana na uwezo wao kiuchumi katika vipengele vyote vya mikopo.
Post a Comment