Ametoa kauli hiyo Ijumaa hii akiwakilisha mada katika kongamano la kumbukumbu ya mwalimu Nyerere lililofanyika katika ukumbi wa chuo kikuu cha kumbukumbu ya mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.
Mzee Butiku, alisema wakati wa TANU mwalimu na viongozi wengine waliweka miiko ya uongozi na kwamba moja kati ya kanuni zake ilikuwa ni kutenga siasa na biashara.
“Katika siasa hivi sasa wanasiasa wote wamekuwa wanajitahidi sana kukataa kanuni hii na wamekuwa wakibabaisha,”alisema Butiku.
“Mjadala wa kutenga siasa na biashara katika zama hizi umekuwa kizungumkuti kwani wanasiasa wengi wamewekeza katika biashara mbalimbali kwa lengo la kujiongezea kipato,”aliongeza.
Post a Comment