0
Muigizaji chipukizi wa filam Tanzania, Evitha Thonest maarufu Jonta ametikisa vichwa vya wengi katika mikoa mbalimbali hapa nchini baada ya kutambulisha movie yake mpya aliyopa jina la Dunia Darasa.

Mwanzoni mwa Septemba mwaka huu, Jonta kupitia ukurasa wake wa facebook amepost kipande cha filam yake mpya ambamo walionekana mastaa kadhaa wa movie akiwemo Dude.


Moja ya post nyingine iliyosisimua wengi ni alipotolea ufafanuzi kuwa amecheza kama mhusika mkuu, na kama haitoshi amehusika na shughli nzima ya kuongoza movie hii mwanzo mwisho.


Uwezo wa Jonta unawashutua wadau wengi wa movie kutokana kwamba ni chipukizi katika uigizaji, na bado hii ni kazi ya kwanza kuiongoza (direct) zaidi ya yote kawashirikisha wasanii wakubwa.

Okaluti-Candle ni msanii wa comedi na mziki wa hip-hop anayewakilisha vyema mkoa wa Arusha chini ya movement ya Like My Light, anadai kuwahi kukaa na Jonta kwa muda mrefu na asijue kama ni msanii.
 Giza mchana.mp3

Okaluti amesema, “Kwanza Jonta nimeiskia juzi tu, mimi namjua kama dada Evi, niliwahi kukaa nae dawati moja primary, kipindi baba amehamishiwa Kagera, na hakuwahi kuonesha dalili zozote za kuigiza”

Ameongezwa kuwa amevutiwa na promo aliyoina facebook kwamba ni ya kusisimua, kufurahisha, kuelimisha na kumshauri Jonta kuzidi kufanya vizuri ili kurudisha hadhi ya bongo movie.

Okaluti amesisitiza, “Jonta wenda ukawa msaada mkubwa kibongobongo, dada evi, fanya km unaongeza maubunifu, ufanye muujiza pekee wa kufufua radha ya movie za tanzania, maana daaah, ila kaza tu”

Dakika Za Madini haikuishia hapo, bali ilifanya bidii ya kuwatafuta wachambuzi wa maswala ya sanaa na kuongea nao ili kupata mtazamo wao wa kitaalam kuhusiana na Jonta wa Dunia Darasa.

Dj DaisyTz wa J.A.C, msimamizi wa kampeni ya Music On Sex! Inayohamasisha wasanii kuzalisha kazi kwa umakini na ubora huku wakilenga katika kuelimisha na kuburudisha jamii naye hakusita kufunguka.

Roho Rehani.mp3

Amesema kuwa kuigiza chanzo chake kikuu ni kipaji, wakati kuongoza chanzo chake ni Taaluma, lazima usomee ndio uweze kufanya hiyo kazi kwa ufanisi unaoweza kuteka hisia za watazamaji.

Daisy amesisitiza, "Mheshim sana mtu anaeweza kuigiza na ku-direct, huyu ni kama madini ya dhahabu, anaweza kuwa mchezoni, akagundua tatizo na kufanya plan b hapo hapo."

Amefafanua kuwa mtu akiweza kuigiza na kuongoza ina maana ana vitu viwili tofauti vinavyoweza kuleta mabadiliko makubwa katika tasnia hii ya filam Tanzania inayochechemea baada ya Kanumba.

Daisy amemaliza kwa kusema, “Cha msingi nipeni contact za huyo Jonta, nitaongea nae kwa undani zaidi then nitawapa mrejesho kuhusiana na uwezo wake katika hii tasnia na ni vip anaweza kuwa msaada.”

Dakika Za Madini inakuja na maelezo matam kuhusiana na Jonta wa Dunia darasa ikishirikiana na Dj DaisyTz, ambapo Jonta atafunguka mengi na kutoa majibu ya hoja zote zinazomhusu.


Post a Comment

 
Top