Waziri mkuu Kassim Majaliwa, ametoa wito kwa waumini wa dini ya kiislamu nchini kutumia sehemu za ibada kuhubiri masuala ya Mungu na sio siasa .
Waziri mkuu ametoa wito huo aliposhiriki sala ya Ijumaa katika msikiti wa Nunge mjini Dodoma na kuwataka waumini wa dini ya Kiislamu kutumia nyumba ya ibada kuhubiri msingi wa dini.
“Niendelee kusisitiza kwamba wote lazima tutumie muda wetu pamoja na mambo mengine lakini pia tumtafute Mungu kupitia nyumba za ibada. Ndugu waislamu wenzangu tufanye kazi ya kuujenga uislamu wetu kwa kuhakikisha kwamba nyumba hizi za dini kuhubiri uislamu,” alisema.
“Kuhubiri msingi wa dini lakini kusisitiza mshikamano miongoni mwetu kuhakikisha kwamba sisi na majirani zetu tunaishi kwa amani na utulivu, ni jukumu letu muhimu sana.”
Post a Comment