0
Naamini katika maisha, huwa inafika mahali kila mtu anatamani akili yake ifanye kazi vizuri na imletee mafanikio makubwa. Lakini hata hivyo, pamoja na matamanio hayo wengi bado huwa hawajui wafanye nini au wachukue hatua zipi ili kuweza kuipa akili nguvu zaidi kila siku na kufanya kazi kwa ufasaha.


Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, baada ya kufanya utafiti kwa muda, walikuja kukaa chini na kuweka vigezo ambavyo kwa mtu akiviafuta basi ni ni lazima akili yake iweze kufanya kazi vizuri zaidi na kwa mafanikio.

Moja ya vigezo walivyoviweka kama unataka akili yako ifanye kazi vizuri ni kama hivi vifuatavyo:- 

1. Chakula bora.
Ili akili yako iweze kufanya kazi vizuri sana, inahitaji kwa kiasi kikubwa chakula bora, chenye virutubisho muhimu. Kwa mfano, tafiti nyingi zilizofanywa kitaalamu zinaonyesha vyakula vya jamii ya samaki ni muhimu sana katika kuipa akili yako afya ya kufanya kazi vizuri.
Hata hivyo utafiti huo haukuishia hapo tu, unazidi kufafanua mara nyingi, watoto wanao tumia vyakula jamii ya samaki sana huwa pia wana uwezekano wa kufanya vizuri hata darasani. Hivyo unaona, chakula bora ni muhimu sana katika kuipa akili yako nguvu ya kufanya kazi vizuri.

2. Mazoezi.
Kati ya kitu rahisi ambacho hakiwezi kukugharimu sana lakini ikiwa utakifanyia kazi na kitaifanya akili yako ifanye kazi vizuri, ni mazoezi. Mazoezi yana uwezo mkubwa sana wa kuipa akili yako nguvu kuliko. Wengi wanaofanya mazoezi, akili zao zipo vizuri.
Unaweza ukachukua jukumu leo la kuifanya akili yako ikafanya kazi vizuri kwa kuamua kufanya mazoezi. Pengine unaanza kuwaza unaanzia wapi? Kama ni hivyo usipate shida. Dakika 20 kwa siku iwe jioni au asubuhi zinakutosha kabisa kuifanya akili yako ikawa na afya bora.

3. Fanya kazi za kujitolea.
Si kila wakati kazi unayofanya ni lazima ikupe malipo. Kuna wakati kubali kujitolea kufanya kazi za jamii tena bure. Unapofanya kazi kama hizi kikawaida kunakufanya ujisiie vizuri na mwisho wa siku akili yako nayo inaanza kufunguka na kufanya kazi vyema hivyo hivyo.
Naona unashangaa katika hili, sikiliza. Wewe ni matokeo ya jamii uliyopo. Kwa mujibu wa kanuni za maumbile ili uweze kufanikiwa ni lazima uirudishie jamii yako kitu fulani kama shukrani. Sasa mojawapo ya vitu hivyo, ndio kazi kama hizi angalau mara moja moja. Ukifanya hivyo ujue kabisa akili itaanza kufanya kazi vyema.

4. Pata usingizi wa kutosha.
Pia usingizi wa kutosha kimetajwa kama ni kigezo kimojawapo cha kuifanya akili yako kufanya kazi vizuri. Inasemakana akili yako ili iweze kufanya kazi vizuri angalau unatakiwa kupata usingizi usiopungua angalau saa nane kwa siku.
Najua hili unalijua vizuri, lakini je huwa unalizingatia? Kama huwa ulizingatia sana, kuanzia sasa litilie mkazo na kuhakikisha lazima akili yako inapumzika na kuipa nguvu ya kufanya kazi vizuri upya kwa siku inayofuata. Ukifanya hivyo ni lazima akili yako ifanya kazi kwa ufasaha, utake au usitake.

5. Jisomee kila siku.
Chakula bora peke yake hakitoshi kuipa akili yako nguvu ya kufanya kazi kwa ufasaha. Kitu cha ziada ambacho kingine unatakiwa kukiongeza ni kujisomea. Akili inayojisomea inakuwa ina nguvu sana ya kufikiria na kufanya mambo kwa ubora.
Najua hili la kujisomea ni shida kwa wengi, lakini hakuna namna nyingine ya kuifanya akili yako ikawa ina nguvu ya kuteda kwa ubora, zaidi ya kujisomea. Unapojisomea unakuwa unaufikirisha ubngo na kuupa changamoto na mwisho wa siku unajikuta umefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana.

Kwa kumalizia makala haya, tambua hayo ndiyo mmbo ya msingi ambayo yamezungumzwa na wataalamu kwamba yanaweza kuipa akili yako nguvu ya kufanya kazi kwa ufasaha.



Nikushukuru ndugu mpekuzi wa DAKIKA ZA MADINI kwa kuungana nami mwanzo mpaka mwisho wa Makala hii, usikose kufatilia makala nyingi za kuelimisha kwa kubofya kipengele cha MADINI. Ulikuwa nami BIN'OTTO THE'OTTONATURE, nikwambie tu, DAKIKA ZA MADINI ndio sehem sahihi ya wewe kupata ujuzi, nasi tuko nawe mpaka ufanikiwe. Kama una tatizo, maoni au ushauri, tuandikie kupitia dakikazamadini@gmail.com





Post a Comment

 
Top