Muimbaji huyo alitumbuiza show mbili za live kwenye uwanja wa Soldier Field, Chicago. Baada ya kujaza siti 89,270, Queen Bey aliingiza $11,279,890 ndani ya siku mbili na alifanikiwa kuuza tiketi 75,106 kwenye show yake iliyofanyika kwenye uwanja wa Stade de France, jijini Paris.
Kwa mujibu wa ripoti ya Billboard imedai kuwa Queen Bey aliuza zaidi ya tiketi 1.8 milioni kwenye show zake 40 alizozifanya ikiwemo huko Marekani, Ufaransa na ile ya Uingereza mwezi uliopita.
Aidha ripoti hiyo imeongeza kuwa muimbaji huyo alifanikiwa kuingiza kiasi cha dola milioni 15.3 kwenye show yake ya Wembley iliyohudhuriwa na mashabiki 142,500 mapema mwezi Julai mwaka huu.
Ziara yake hiyo inatarajiwa kufikia tamati October 2, 2016.
Post a Comment