0
Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,
Josephat Gwajima
POLISI Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limeshamhoji Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima na kuandika maelezo.

Limesema kwa sasa linaendelea na upelelezi ; na endapo atapatikana na hatia kuwa alitoa maneno ya uchochezi, yaliyosambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii, watamfikisha mahakamani kwa hatua zaidi.

Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kukamatwa kwa Gwajima.



Sirro alisema walimkamata Gwajima kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) juzi wakati aliporejea nchini kutokea Japan.

Askofu Gwajima alikuwa anatafutwa na jeshi hilo kwa ajili ya kuhojiwa juu ya mahubiri yake, aliyoyatoa Juni 11, mwaka huu kanisani kwake Ubungo Maji jijini Dar es Salaam.

Katika mahubiri hayo ambayo yalisambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii, askofu huyo alisikika akiukosoa utendaji kazi wa Rais mstaafu, Jakaya Kikwete.

Pia Gwajima alisikika akimshauri Rais John Magufuli, kuhama Chama Cha Mapinduzi (CCM) iwapo watakataa kumkabidhi uenyekiti wa taifa na kwamba apeleke muswada bungeni, kuondoa kinga ili rais ashtakiwe kwa makosa aliyoyafanya akiwa madarakani.

Post a Comment

 
Top