0
Jeshi linataka shamba hilo ligeuzwe kuwa makaburi

Mzozo umezuka nchini Pakistan kuhusu shamba ambapo kiongozi wa zamani wa mtandao wa al-Qaeda Osama bin Laden alikuwa anaishi mjini Abbottabad.

Bin Laden aliuawa kwenye shambulio lililotekelezwa na wanajeshi wa Marekani katika shamba hilo Mei 2011.

Maafisa wa jiji wanataka kugeuza shamba hilo kuwa uwanja wa kuchezea watoto.



Hata hivyo, jeshi linataka kipande hicho cha ardhi kigeuzwe na kuwa makaburi.

Kuna baadhi ya wakazi wanaotaka shamba hilo litumiwe kujenga shule ya wasichana huku baadhi ya wanajeshi nao wakitaka ligeuzwe kuwa bustani ya burudani na kutumiwa kuzalisha mapato kwa serikali.


  • Kanda za sauti ya Osama zasikika
  • Mkwewe Bin Laden maisha jela
  • Osama aliacha dola milioni 29 kufadhili Jihad


Huku mzozo kuhusu pande hizo mbili ukiendelea, jeshi mnamo Jumatano lilifika na kujenga ua, jambo lililoshangaza maafisa wa baraza la jiji.

Bin Laden aliishi kwenye jumba la ghorofa tatu lililo kwenye shamba hilo bila kujulikana kwa miaka kadha. Jumba hilo lilikuwa limezungushwa ua mrefu.

Shamba hilo, lenye ukubwa wa mita 3,530 mraba na linalokadiriwa kuwa na thamani ya $285,000 (£218,000), limekuwa wazi tangu wakati huo.

Baada ya kifo cha Bin Laden, shamba hilo lilikabidhiwa serikali ya jimbo la Khyber Pakhtunkhwa (KP) pambayo ilibomoa jumba hilo pamoja na ua ili kuzuia eneo hilo lisigeuzwe na wapiganaji wa kijihadi kuwa eneo 'takatifu'.

Post a Comment

 
Top