Taarifa kutoka nchini Saudi Arabia zinasema kuwa mshambuliaji wa kujitolea mhanga amejilipua karibu na tawi la ubalozi wa marekani katika mji wa Jedda.
Ripoti zinasema kwa ni mshambuliaji tu aliyeuawa lakini baadhi ya taarifa zinasema kuwa walinzi wawili walijeruhiwa na shambulizi hilo.
Shambuli kwenye tawi la ubalozi wa marekani mjini Jedda mwaka 2004 lilisababisha vifo vya watu 10.
Wakati huo huo utawala nchini Kuwait unasema umetibua mashambulizi matatu yaliyokuwa yamepangwa na kundi la Islamic State likiwemo lililokuwa limelenga msikiti wa washia.
Wizara wa mambo ya ndani inasema kuwa idara za ulinzi ziliendesha oparesheni tatu ndani ya Kuwait na nje, ambapo watu kadha walikamatwa.
Mwaka uliopita mshambuliaji wa kujitolea mhanga raia wa Saudi Arabia aliwaua watu 27 wakati alijilipua ndani ya msikiti wa washia nchini Kuwait.
Post a Comment