0
Baadhi ya majeruhi wapo katika hali
mbaya na hospitali za eneo hilo zinahitaji
msaada zaidi wa damu.
Juhudi za uokoaji zinaendelea kusini mwa Italia eneo ilipotokea ajali ya treni ambapo watu 23 wamefariki na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa.

Treni mbili ziligongana karibia na mji wa Andria,Kaskazini Magharibi mwa mji wa Bari.

Baadhi ya majeruhi wapo katika hali mbaya na hospitali za eneo hilo zinahitaji msaada zaidi wa damu.

Vyombo vya habari vinasema mfumo wa breki ulishindwa kufanya kazi katika treni moja wapo na kusababisha kugongana na nyingine,huku taarifa nyingine zikisema ilikuwa ni makosa ya kibinaadamu.



Papa Francis ametuma salamu za rambirambi sambamba na kufanya maombi kwa wahanga na familia zao

Post a Comment

 
Top