Shirika la Amnesty International imezituhumu Mamlaka nchini Misri kuhusika na kupotea kwa watu, kwa lengo la kutishia upinzani.
Katika ripoti mpya, Shirika hilo la Kutetea haki za Binadamu limethibitisha kwa nyaraka, kupotea kwa watu tangu mwanzoni mwa mwaka 2015.
Ripoti hiyo inasema mamia ya wanafunzi, wanaharakati wa masuala ya siasa na waandamanaji huku wengine wakiwa vijana zaidi kama umri wa miaka 14 wametoweka mpaka sasa bila ya kujulikana walipo.
Ripoti hiyo mpya ya Amnesty International pia inasema watu watatu mpaka wanne wanakamatwa na vyombo vya usalama kila siku na wengine wamekuwa wakishikiliwa kwa miezi.
Imevilaumu pia vyombo vya kimahakama kuhusika katika kupotea kwa watu hao.
Post a Comment