0

Wanafunzi elfu saba (7800) waliokuwa wamejiunga na chuo kikuu cha Dodoma Tanzania ni wanafunzi 382 pekee wenye sifa zitakazowaruhusu kurejea chuoni humo.



Waziri wa elimu sayansi na teknolojia Pof. Joyce Lazaro Ndalichako aliwaambia wanahabari jijini Dar es Salaam kuwa baada ya uchambuzi wa sifa za wanafunzi 7,800 waliofukuzwa, idadi ya wanafunzi ambao wana sifa za kuendelea na masomo ni 382.

Prof. Joyce Ndalichako alisema kuwa kozi hiyo maalum iliyolenga kusuluhisha uhaba wa walimu wa sayansi katika shule za upili nchini Tanzania ilikuwa na wanafunzi 1,210 ambao walikuwa wanasomea stashahada ya ualimu wa shule za msingi.

Vilevile wanafunzi 6,595 walikuwa wanasomea stashahada ya kufundisha shule za sekondari.
Kufuatia uchunguzi huo Prof. Ndalichako alitangaza orodha ya wanafunzi watakaorejea katika chuo kikuu cha Dodoma (UDOM).

Sifa zilizotakiwa ni ufaulu wa daraja la 1 hadi daraja la 3 na krediti mbili au zaidi katika masomo ya Sayansi na Hisabati,
“Kati ya wanafunzi wanaosomea ualimu wa sekondari 6,595 ni wanafunzi 382 pekee ndiyo wana sifa za kuendelea na masomo hayo, 134 ni mwaka wa kwanza na 248 ni mwaka wa pili,” Prof. Ndalichako.

Na si hayo tu wanafunzi 4,586 wa mwaka wa kwanza wa kozi hiyo maalum wa stashahada ya ualimu wa sekondari waliokidhi vigezo vya ufaulu watahamishiwa katika vyuo vya ualimu vya serikali ambayo ni Tukuyu Butimba, Songea Morogoro, na Mpwapwa.

Aidha wanafunzi 1,337 wa mwaka wa pili watahamishiwa vyuo vya Kasulu na Korogwe iliwaendelee na masomo yao.
Wanafunzi wa UDOM watarejea chuoni mwezi Oktoba mwaka huu.

Post a Comment

 
Top