Upekee wa Mlima OL DOINYO LENGAI 12:35:00 AM Unknown 0 FAHARI A+ A- Print Email Ol Doinyo Lengai (Kimaasai "mlima wa Mungu") ni mlima wa volkeno katika Tanzania ya Kaskazini. Iko takriban 120 km kaskazini-magharibi ya Arusha. Iko 25 km kusini ya Ziwa la Magadi (Tanzania - "Lake Natron"). Jina la mlima ni Kimaasai lamaanisha "mlima wa Mungu". Mlima una kimo cha 2690 m juu ya UB. Ni volkeno ya pekee duniani kutokana na aina ya lava yake inayotoka hali ya kiowevu (majimaji) lakini si moto sana (mnamo 500° - 600 °C). Ol Doinyo Lengai ililipuka tena Machi 2006. Katika mwaka 2007 mlima umesababisha mitetemeko ya ardhi ya mara kwa mara kuanzia 12 Julai. Tetemeko la 18 Julai lilisikika hadi Nairobi.
Post a Comment