Habari mpenzi…. Ndugu na Jirani wa Madini Media…!
Nafurahi
tumekutana ili tuweze kuangazia kwa undani maswala yanayogusa maisha yetu.
Ndugu, lini umewahi kujiuliza kuhusu Hali yako, umuhimu wako, malengo yako,
hatima yako, changamoto zako na mengine kama hayo kwako binafsi na katika jamii
kwa ujumla.
Unakumbuka
siku ulipoambiwa kuwa, “Mbona haujitambui wewe,
hata hujielewi?”. Tamkini
aliyekutamkia maneno hayo kwa muda huo alimwona kama adui ingawaje baada ya
siku mbili tatu ukamsamehe na kupotezea, baada ya hasira kupungua au kuisha.
Kumbe
suluhisho ilikuwa sio kukasirika, bali kujitathimini kwanza na kutafakari sana
chanzo cha kuambiwa hivo, ndipo uchukue hatua ya kujiridhisha kuwa ni kweli una
kasoro au yeye msemaji ndio hajitambui. Ukiweza kufanya hayo yote ndipo
tutasema unajitambua.
Wengi
walitamani sana kujipima katika utendaji wao, usemaji wao na hata viwango vyao
katika kuwaza, wakahisi kwa “Kuwauliza wenzao” watafaulu, na matokeo
yakaangukia sifuri. Ndio maana leo nipo nawe ili matokeo yako yaangukie mia.
Tuungane…
MBINU ZITAKAZOKUWEZESHA KUJITAMBUA
1.
PIMA UMRI NA KIWANGO CHA FIKRA ZAKO
Sote
tunafahamu kuwa hakuna kiwango maalumu cha kufikiri kilichoidhinishwa kimataifa
kutoka umri mmoja na mwingine. Bali tunaviwango vya kimataifa vinavyotoa uwiano
wa umri wa mtoto na kuandikishwa shule.Hata hivyo kuna uwezekano mkubwa wa
kupima kiwango cha fikra zako kwa kulinganisha na umri wako.
Unaweza
kupima fikra zako kwa kutazama ubora wa matokeo ya kila unachoamua kutenda
pasipo kusaidiwa na mtu mwingine. Pia unaweza kupima fikra zako kwa
kuzilinganisha na ubora wa fikra za watu wenye kiwango cha juu cha fikra katika
umri wako. Lakini mwisho wa yote viwango bora kabisa vya kifikra vinalenga juu
ya usahii wa wakati katika kutekeleza jambo fulani.
Unaweza
kupima jinsi unavyopanga,unavyoamua,unavyotekeleza, na kuendelea au kusitisha
maswala fulani fulani katika maisha yako na aina ya matokeo unayoyapata kwa
kuzingatia ubora wake. Kwa kufanya hivyo itakusaidia kuanza kupata picha ya
namna gani unajitambua.
2.
TAFUTA KUJUA UPEKEE ULIONAO
Hii
nayo ni kati ya mbinu bora inayokufanya ujitambue. Watu wengi hupenda kufanana
na watu fulani fulani haswa watu ambao wao huwaita role model (mtu wa mfano), Na
kusahau kuwa yeye ndiye role model na.1 kwake binafsi.Makosa haya humpelekea
mtu huyo kujua zaidi kuhusu huyo role model na.2 na upekee wake kuliko
anavyoweza kujifahamu mwenyewe.
Leo
imekuwa ni kawaida kumsikia mtu akieleza kwa ufasaa upekee alionao OBAMA na
MKEWE lakini ukimuuliza upekee alionao akakujibu kirahisi tuu sijui. Kitu pekee
kitakachokuokoa na tatizo hili ni kuamua kufahamu upekee ulionao na si upekee
wa mtu mwingine au Role model wako.
Kama
wewe ni mwandishi wa vitabu jiulize unatofautiana nini na waandishi wengine,au
kama ni mwanafunzi, mwanasayansi, mchezaji, mwanajamii, nk, unatofauti gani na
wengine ukiwa na maana uthamani wako uko wapi zaidi.
3.
TAFUTA KUJUA CHANGAMOTO ZINAZOKUKABILI
Kama
kweli umedhamiria kujitambua unatakiwa kufahamu changamoto au matatizo
yanayokukabili.Changamoto hizo zinaweza kuwa ni zile zinazotokana na rika, mazingira,
kiwango cha elimu yako,Hali uliyonayo (ulemavu, mahitaji maalumu au uathirika
wa magonjwa, ndoa, bila ndoasingle nk.).
Kama
ni rika tambua rika lako linakabiliwa na changamoto zipi.Ikiwa ni mazingira
tafuta kujua changamoto za kimazingira ulizonazo. Unaishi kijijini, mjini, shuleni,
chuoni, mfanyakazi, kiongozi, mfuasi au vinginevyo, jiulize katika mazingira
hayo unakabiliwa na changamoto gani. Inawezekana wewe ni teenager (13-19 miaka)
au kijana au mzee, jiulize kuhusu changamoto zako.Vivyo hivyo kwa kiwango cha
elimu pamoja na hali kama ilivyofafanuliwa katika mabano.Orodhesha changamoto
zinazokukabili.
Kumbuka
hata uonevu wa kibinadamu wa kawaida hutokea zaidi kwa watu wasiozingatia
kipengele hiki cha ufahamu wa changamoto. Hakikisha unafahamu wapi utakwama
kabla hujafikia na kuanza kuchukua hatua mapema iwezekanavyo.kitendo hicho
kitakufanya uwe macho saa zote na kila atakayekuona atakuthamini hivyo kutokuwa
na madhara kwako.
4.
TAFUTA KUJUA WAJIBU NA MAJUKUMU YA WATU WA RIKA LAKO
Kwa
haraka unaweza kufikiri kuwa nataka kufundisha uraia.Utanisamehe kama nitakuwa
nimekukumbusha kitu unachoimba au ulichoimba kilasiku shuleni.Lengo langu
nataka nikufumbue macho kuhusu wajibu na majukumu kama dhana muhimu katika
kujitambua.
Hadithi:
Mama mmoja alikuwa akilia kwa uchungu nje ya nyumba
yake huku akijitupatupa chini na kugalagala. Majirani wakaja mbio na
kukusanyika kufahamu kilichotokea.Lakini kila walipomuuliza mama alichokua
akililia aliwaonyesha kidole katika mlango uliokuwa wazi.
Watu wakakimbilia ndani na kumkuta mtoto wa miaka minne na nusu
aliyewekewa kila kikorokoro cha kuchezea lakini hakuna alichokishika wala
kukichezea. Walipotoka na kumuuliza mama mbona hatukuona chochote zaidi ya
mtoto na vitu,mama akaongeza kilio na kusema
“masikini mwanangu hasala gani hii!
huyu ni mwanangu watatu, wenzake waliotangulia walikufa kwa moto shambani
kwasababu hawakuweza kusogea hata hatua moja moto ulipotokea nilipokuwa
kisimani kuteka maji.kinachoniumiza zaidi ni kuona hata huyu naye hagusi
chochote nilichomwekea nahisi naye atakufa kifo kama cha wenzake”.
Kwa
mfano huo tunapata picha ya mtu asiyetambua wajibu wake anavyoweza kuleta
hasara kubwa kwake yeye mwenyewe ,kwa familia yake na kwa taifa lake.Mama
aligundua kuwa mtoto wake hajitambui kwa kutonyanyua chochote.majukumu ya
msingi ya mtoto wa umri ule ni kucheza. Kutokucheza ilikuwa ni ishara tosha ya
kutokujitambua. Je wewe ni mmoja wa wale wasiowajibika?.
Piga picha
na kuyatazama majukumu yako kama mtoto, kijana au mzee.
- · Jiulize kuwa wewe ni Yule mtoto mwenye kila kilicho mbele yake lakini hakuna anachogusa?.
- · Jiulize kuwa umekuwa mtu wa kunyooshea vidole majukumu au umekuwa mstari wa mbele kutumikia?.
- · Umewahi kushiriki kutatua kero yeyote nyumbani kwako ,mtaani kwako au maeneo yaliyokuzunguka?
- · Jiulize unafanya nini katika kujiandaa kutumia fursa zinazojitokeza duniani?
- · Nafasi uliyonayo unaitumia kufanya wengine kuinuka au unawadidimiza?
- · Jiulize kama wewe ukikosekana duniani, dunia itakuwa imepata hasara yeyote?
Wakati
unajiuliza maswali hayo ni wazi kuwa utaanza kupata picha ya jinsi ulivyo kwa
kupima uwajibikaji wako.Kitendo kicho kitakufanya uongeze uelewa wako juu yako
binafsi na kwasababu hiyo utaingia kwenye kundi la watu wanaojitambua.
5.
PIMA KUJIAMINI KWAKO
Ili
kujitambua inakupasa kuchukua jukumu hili msingi la kupima kujiamini kwako.Hebu
jichukue katika fikra zako na kujiweka mbele ya umati mkubwa wa watu wenye
uelewa wa kutosha.Jaribu kuwaelezea au kuonyesha kitu ambacho unakifahamu kwa
usahihi kabisa hapa duniani. Unahisi unaweza kukifanya kikamilifu bila hofu wala
kubabaika.
- · Unaweza kujikumbusha mambo ambayo yalikuwa yanakufanya ushindwe kujiamini kama bado yapo au la.
- · Pima ubora wa unachofanya kama una nafasi yeyote katika viwango vya kidunia?.
- · Kama wewe unajihusisha na sanaa je sanaa yako inaweza kumvutia mtu yeyote duniani?.
- · kama ni huduma je! huduma yako inaweza kumfaa mtu yeyote duniani?
- · Kama ni mwanafunzi je wewe unaweza kuwa mwanafunzi bora popote duniani au ni hapo kijijini kwako tu?.
- · Unaweza kushindanishwa na mtu yeyote duniani kwa hilo ambalo wewe ni bora sana hapo kwenu au ubora huo ni wa hapo kwenu tu?.
Kwa
vipimo hivyo vitakufanya uzidi kujitambua na kuchukua hatua ya kuondosha
mapungufu uliyonayo na kukufanya uzidi kujiamini.
6.
WEKA VIPINDI MAALUMU VYA KUJITATHIMINI
Kitendo
cha kujitathimini kitakufanya kujichunguza na kujiweka karibu na wewe
binafsi.Tatizo kubwa tulilonalo leo duniani ni kwamba tunawatu wengi ambao wako
karibu sana na watu wengine lakini hawako karibu na wao wenyewe. Kifupi ni
kwamba wanajua sana kinachoendelea kwa watu wengine kuliko kinachoendelea kwao
binafsi.
- · Wanalaumu watu hawana elimu wakati wenyewe hawana,
- · Wanatetea unyanyasaji wa kijinsia wakati wao wenyewe wananyanyaswa,
- · Wanalaumu watu wanaovunja ndoa wakati wao wenyewe wana nyumba ndogo,
- · Wanalaumu kuhusu wizi wa viongozi wa umma wakati Wao mwenyewe wanaiba kwenye kampuni zao.
Sasa,
kitu ambacho kinaweza kusaidia katika kujitambua ni kufanya tathmini binafsi
juu ya mwenendo wako. Kabla hatujaanza kukosoa uzembe wa watu wengine tenga vipindi
maalumu ikiwa ni kila baada ya wiki,mwezi au mwaka kutathimini ni uzembe wa
namna gani umefanya na matokeo yake.Hata hivyo unaweza kufanya tathimini za
kila siku ili kutokuwa na mlundikoano wa tafakuri za muda mrefu kuhusu namna
ulivyoishi.
Unaweza
kutathimini kiwango cha mafanikio kwa kulinganisha na matarajio,kiwango cha
mapungufu kwa kwa kulinganisha na namna ulivyoshindwa.Kama mafanikio
hayakufikia malengo basi ni wazi kuwa bidii na mbinu bora zaidi zinahitajika na
kama matokeo ni kushindwa basi ni wazi kuwa mfumo mzima wa maisha inabidi
ubadilike na mbinu mpya zinatakiwa.
Kiwango
cha kujitambua kinaendana na tathimini binafsi. Ni kiwango cha hali ya juu cha
kutojitambua kuendelea na kazi ileile au mbinu ileile inayokufanya kilasiku
ushindwe kutimiza malengo yako.Kila baada ya tathimini lazima uje na
mapendekezo mapya yenye mbinu mpya ,mikakati mipya na matarajio mapya.Kwa
kufanya hivyo ni dhahili kuwa kiwango chako cha kujitambua kitakua na kuongeza
mabadiliko ya kila siku katika maisha yako.
7.
KUBALI KUANZA UPYA
Bila
kujali wasifu ulionao unaweza kuonyesha kiwango cha kujitambua kwako kwa kuanza
upya mara tu unapobaini kuwa kunamakosa makubwa katika mwenendo wa maisha yako.
Mtu mwenye kiwango cha chini kabisa cha kujitambua hawezi kuanza upya, kwasababu
ya kutojitambua kwake haoni shida kwa lolote limpatalo na kuhisi kuwa
amestahili.
Mtu
asiyejitambua haoni umuhimu wa kubadilisha mtindo wa maisha kwasababu hufikiri
kuwa kufanya hivyo ni sawa na kupoteza wakati. Inashangaza sana kumwona mtu
anatumia staili ya aina moja katika kupambana na changamoto ambazo kila siku
zinabadilika.
Jenga
tabia ya kukubali kuanza upya kila unapoona kuwa hatua ya kiwango cha makosa
ulichofikia hakiwezi kurekebishika.mfano ,kama pengine fani unayoitumikia
haiendani kabisa na kipaji ulichonacho kubali kuanza kujifunza fani nyingine. Na
endapo marafiki ulionao wanakusababisha kushindwa kutimiza majukumu yako,
kubali kuanza kutafuta marafiki wapya.
Kitendo
cha kukubali kuanza upya ndipo ulipo mfupa mgumu ulomshinda fisi, ila kumbuka
wewe unayo maarifa akili na uwezo zaidi ya wanyama wote, hivo sina shaka na
wewe katika hili. Utakapoanza awamu ya pili itakusaidia kubaini makosa
uliyoyafanya mwanzo na kwasababu hiyo kuwa mwalimu wa wengine.
Naamini
hizi dakika kadhaa ulizosalia nami zimekulisha ubongo wako MADINI ya kutosha
nayo itakuwa ni kumbukumbu kwako siku zote. Usikubali haya yabaki tu akilini,
jitahidi kuyafanyia kazi ili
uwezekupokea matokeo chanya katika maisha yako.
Yamkini wewe
umekuwa moja ya wengi wanaoshangaa kiwango cha upendo nilichonacho hata kugawa MADINI bure, usijali, mwenyewe kufikia hapa kuna wengi
walijitoa kwa ajili yangu nami nafanya vivyo hivyo kila siku kupitia MADINI MEDIA.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.