Taarifa hiyo ya Ikulu haikueleza sababu za kutenguliwa kwa uteuzi huo, lakini ni siku moja tangu Mwele kueleza kuwa ugonjwa wa zika upo nchini.
Taarifa iliyotolewa usiku huu na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa inasema uteuzi wa mkurugenzi mpya atakayejaza nafasi hiyo utatangazwa baadaye.
Akizungumza na waandishi wa habari juzi Alhamisi, Dk Malecela alisema kati ya watu 533 waliopimwa wakati wa utafiti walioufanya, asilimia 15.6 waligunduliwa kuwa na virusi vya zika.
Hata hivyo, siku moja baadaye, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alikanusha uwapo kwa virusi hivyo.
“Kama nilivyoeleza Februari, ugonjwa huu haujaingia nchini, napenda kuwatoa hofu wananchi, hivi sasa Tanzania haujathibitishwa kuwapo na ugonjwa wa zika,” alisema Ummy Mwalimu.
Wizara hiyo inasema uchunguzi uliofanywa na NIMR ulikuwa wa kuchunguza ubora wa kipimo kipya cha kupima magonjwa ya Zika na Chikungunya.
Taarifa za kuwapo ugonjwa wa zika nchini zimewavuruga viongozi wa Wizara ya Afya na Taasisi ya Utafiti wa Tiba na Magonjwa ya Binadamu nchini (NIMR) baada ya jana Ijumaa kujitokeza kuzikanusha.
Katika mkutano na waandishi wa habari, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Dk Mwele Malecela alisema huenda wanahabari hawakumwelewa huku Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Maendeleo ya Jamii, Ummy Mwalimu akisema taarifa za kuwapo ugonjwa huo hazikufuata utaratibu na hazijathibitishwa.
Post a Comment