Baada ya hivi karibuni kuenea habari kuwa mchungaji wa kanisa la Maombezi, Anthony Lusekelo amemfanyia fujo jirani yake hivyo kushikiliwa na polisi na kwamba alionekana akiwa amelewa pombe, ameibuka na kuwaonya wale wanaozusha habari za uongo.
Akiwahubiria waumini wake Jumapili hii, Mchungaji huyo alisema, “Wiki iliyopita nilikuwa wizara ya mambo ya ndani, baadhi ya maofisa wakaniona, wewe mzee wa upako, wewe mzee wa upako, askari mmoja akaniuliza unachukua sadaka unaenda kunywa pombe. Nikawauliza hiyo pombe nilikunywa wapi, halafu pombe zipo nyingi, taja ni pombe gani, ukienda mbali zaidi ungeuliza nililewa nini, maana hata upako wa roho mtakatifu ni ulevi.”
Mchungaji huyo aliongeza kuwa hakuna binadamu atakayeweza kumwangusha kwa kipawa na karama aliyopewa na Mungu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment