0
Karibu ukaribie mwanamichezo mwenzangu katika site yako uipendayo ya MADINI MEDIA. Leo ni siku njema ambayo nitakurudisha nyuma kibabe hata kama una nguvu au hautaki, na zaidi utacheka badala ya kuchukia. Nakurudisha nyuma kivipi? Yaani utotoni, Kivipi? Je unakumbuka kipindi upo awali na shule ya msingi ukicheza mpira wa makamba?



Binafsi nafurahi sana sababu umekumbuka. Katika maisha ya kawaida unaweza kuwa unabanwa au unafuata sheria bila kuitambua. Najua unajua na unazijua sheria 11 za mpara wa miguu. Lakini hizi ni tofauti kabisa na zile za mpira wa makamba.


ZIPO SHERIA 16 ZA MPIRA WA UTOTONI NAZO NI KAMA IFUATAVYO:

1.Mwenye mpira Lazima acheze hata kama hajui kucheza

2.Dogo mnene Lazima awe golikipa

3.Mwenye mpira ataamua nan acheze na nan asicheze

4.kama haujashiriki kufuma mpira unaweza usipate namba

5.idadi ya wachezaji inategemeana na uwanja

6.Mwenye mpira akikasirika mpira umeisha

7.Inaruhusiwa kubadili golikipa kama ikitokea penat na baada ya hapo ataendelea kudaka yule yule golikipa

8.Mechi itaisha pale giza linapoingia

9.Wale ambao wamekosa namba kazi yao ni kufata mpira ukitoka

10.Hakuna half-time wala offside maana hauna refa!

11.Kama umevaa viatu uvue

12.Hakuna jezi, wengine wavue mashati wengine wavae.

13.Mtaalam Wa Timu Akipewa Kazi Na Wazazi Wake Lazima Mumsaidie Ndo Mwende Kucheza.

14.Penati Itatokea Tu Pale Mchezaji Akiumia Sana Na Kutoka Damu.

15.Mechi Itaisha Kama Kila Mchezaji Atakuwa Amechoka.

16.Ukiumia Kidonda Kinawekwa Mchanga.

Warap, ulikuwa nami mwanamichezo ninaecheza kama madensa wa Michael Jackson nikiwa uwanjani, niite BIN'OTTO THE'OTTONATURE. Usikose kutembelea MADINI MEDIA, kwa HABARI, MICHEZO NA BURUDANI, lakini pia kwenye kipengele cha MADINI unapata kujisomea makala zitakazokuwezesha kufanikiwa kimaisha.

Post a Comment

 
Top