0
WAKALA wa Jiolojia Tanzania (GST), imetoa ufafanuzi kuhusu tetemeko lililotokea mkoani Kagera. GST imesema, kitovu cha tetemeko hilo kiko chini ya ardhi urefu wa kilometa 10.


Imetoa tahahadhari kwa wananchi kuepuka madhara yanayoweza kusababishwa na tetemeko la ardhi kabla, wakati na baada ya tukio ili kupunguza madhara yanaweza kutokea.


Imesema, jamii inastahili kuelimishwa kuhusu tahadhari ili kila mmoja aelewe nini cha kufanya linapotokea tetemeko la ardhi ikiwa ni pamoja na kupata mafunzo kutoka kwa watu wa Chama Cha Msalaba Mwekundu kuhusu namna ya kuhudumia majeruhi.

GST pia imesema, Jeshi la Zimamoto linapaswa kuwaelimisha wananchi ili wafahamu namna na kutumia vifaa vya kuzimia moto.

Wananchi wanashauriwa kujenga nyumba bora na imara kwa kuzingatia viwango vya ujenzi ikiwa ni pamoja na kuweka misingi imara na kupata ushauri wa kitaalamu wa aina ya majengo yanayofaa kujengwa katika eneo husika kulingana na ardhi ya mahali husika.

GST imesema, wakati wa tetemeko wananchi wanashauriwa kukaa mahali salama kama vile sehemu ya wazi isiyo na majengo marefu, miti mirefu na miinuko mikali ya ardhi

Post a Comment

 
Top