Watangazaji hao wamepewa muda wa mwezi mmoja kupunguza uzito wa mwili
Televisheni ya taifa nchini Misri imewafukuza kazi wafanyakazi 8 wa kike na kuwashauri waende wapunguze uzito wa mwili.
Chama cha Radio na Televisheni nchini Misri ( ERTU) kimewapa wanawake hao muda wa mwezi mmoja kupunguza uzito kabla ya kuruhusiwa kuonekana tena kwenye televisheni.
Mkurugenzi wa ERTU ni mwanamke, Safaa Hegazy na ambaye wakati mmoja alikuwa mwenyewe ni mtangazaji wa runinga. Tangazo hilo limezua lawama kutoka kwa watangazaji walioathiriwa.
Mmoja wao Khadija Khattab, mtangazaji wa kituo cha Channel 2, alisema kuwa anataka watu kutizama kipindia chake na kujiamlia wenyewe ikiwa ana uzito wa juu.
Post a Comment