Naibu Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam, Hezron Gyimbi amesema Ijumaa hii kuwa fedha hizo zimekusanywa kupitia kikosi cha usalama barabarani baada ya kukamata magari kwa makosa mbalimbali ya usalama.
“Idadi ya magari yaliyokamatwa ni 39,280, pikipiki 2,382, daladala 16,739, magari binafsi na malori 22,541 na jumla ya madereva pikipiki 12 wamefikishwa mahakamani kwa makosa ya kutovaa kofia ngumu na kupakia zaidi ya abiria mmoja, maarufu kama mishkaki,” alisema.
Aidha Katika tukio jingine, jeshi hilo limekamata gari la wizi aina ya Fuso lenye namba ya usajili T 619 BTG lenye thamani ya shilingi milioni 50.
Aliendelea kutoa ufafanuzi wa gari lililoibiwa kuwa gari hilo Lilikuwa limebadilishwa namba na kuweka T 262 CBC Alisema gari hilo lilikamatwa kupitia kikosi cha kupambana na wizi wa magari ya Mkoa wa Kipolisi wa Kimara iliyoibiwa Julai 25 katika ofisi za kufyatulia matofali eneo la Kimara, mali ya Richard Bernard (36) mfanyabiashara mkazi wa Luguruni, Mbezi katika Manispaa ya Kinondoni.
Makusanyo ya fedha hizo ni kuanzia Julai 29 hadi Agosti 11, mwaka huu na kukusanya fedha hizo .
BY: EMMY MWAIPOPO
Post a Comment