0
MSHINDI wa tuzo za Oscar nchini Marekani raia wa Kenya, Lupita Nyong’o, ameamua kumweka wazi mpenzi wake, Mobolaji Dawodu, ambaye ni mwanamitindo mwenye asili ya Nigeria.


Wawili hao walianza uhusiano wao miezi sita iliyopita na sasa wameamua kuweka wazi uhusiano wao huo, baada ya kuona wanafanana kwa baadhi ya vitu walivyochunguzana.


Kupitia akaunti ya Instagram, Lupita aliweka picha mbili akiwa na mwanamitindo huyo, huku akidai kwamba huo ndio muda mwafaka wa kuweka wazi mambo yao ya siri.

“Kila kitu kina wakati wake, tumekuwa karibu kwa miezi sita iliyopita, nadhani sasa ni wakati sahihi wa kuweka wazi nini kinaendelea kati yetu, nampenda na ananipenda,” aliandika Lupita.

Post a Comment

 
Top