0
Rapper Darassa alipata fursa ya kuwazungumzia wazazi wake kwenye kipindi cha Ngaz Kwa Ngaz cha EATV kinachoendeshwa na Salama Jabir.


“Wazazi wangu wako hai wote wawili lakini for years tangu mimi hapa nimezaliwa hawajawahi kuwa wanaishi pamoja,” alisema Darassa kwenye kipindi hicho.


“So asilimia kubwa mimi nimelelewa na bibi yangu, mama yangu, na marehemu dada yangu,” aliongeza.

Kuhusu jina lake Darassa, alidai kuwa alilipata kitambo enzi marehemu Complex yupo hai ambapo alienda kwenye studio zake na kuwakuta watu waliokuwa wakirekodi. Anasema watu hao walionekana kukosea baadhi ya vitu na yeye kuwashauri njia nzuri na hivyo kupelekea kumpa jina ‘Darassa.’

Kwa sasa rapper huyo anafanya vizuri na wimbo wake ‘Too Much.’

Post a Comment

 
Top