0
Baada ya vocalist, Rich Mavoko kusaini WCB ya Diamond, huwenda msanii muziki wa R&B kutoka Morogoro, Belle 9 na yeye akasaini ndani ya label hiyo.



Muimbaji huyo anayefanya vizuri na wimbo ‘Bugger Movie Selfie’ ameonekana akifanya mazoezi ya bendi ya Diamond katika ofisi za WCB.


Kwa mujibu wa kipindi cha Planet Bongo cha EATV, Belle pamoja na Diamond wameonekana wakiimba wimbo ‘Mdogo Mdogo’ kwa pamoja huku wakicheza.

Hatua hiyo imefufua matumaini mapya kwa mashabiki wa kumuziki kuona huweza WCB ikamsaini msanii hiyo kama ilivyofanya kwa Rich Mavoko.

Kwa sasa label ya WCB ina wasanii wanne, Harmonize, Rich Mavoko, Raymond aka Rayvany pamoja Queen Darlin.

Post a Comment

 
Top