0
Jaji Ginsburg amesema anajutia aliyoyasema


Jaji mmoja wa Mahakama ya Juu zaidi ya Marekani ameomba radhi kwa matamshi yake ya hadharani ya kumshtumu mgombea kiti cha urais kwa tiketi ya Republican Donald Trump.



Jaji huyo Bi Ruth Bader Ginsburg amejikosoa kwa matamshi hayo ambayo anasema anayajutia.

Trump amekuwa akimtaka Jaji Ginsburg ajiuzulu

Katika msururu wa mahojiano na vyombo vya habari Jaji Ruth Bader Ginsburg amekuwa akimuelezea Bw Trump kama mtu asiye na sifa njema, mwenye majivuno yasiyofaa na aliye na tabia zisizostahili kwa rais.

Katika kujibu kauli hizo Bw Trump amekuwa akisema jaji huyo anapaswa kujiuzulu kwa sababu ni makosa kwa mtu mwenye wadhifa wake kujiingiza katika kampeni za kisiasa.

Post a Comment

 
Top